Zanzibar:Shein akutana na Maalim Seif
Mazungumzo ya
kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano
uliowaleta pamoja rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad ukifanyika.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini
Tanzania, mkutano huo wa faragha katika ikulu ya rais ulihudhuriwa na
marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid karume.
Ni mara
ya kwanza kwa Dkt Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw
Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni makamu wa rais wa kisiwa
hicho kukutana tangu tume ya uchaguzi.
Kushirikishwa kwa marais hao
wa zamani ni thibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa zinazoendelea
katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua mgogoro wa
kikatiba.
Wanachama wa jumuiya ya kimataifa pia wanadaiwa kushiriki katika kumaliza tatizo hilo.
Hakuna
habari zilizotolewa kutoka pande zote mbili lakini duru za serikali
zimethibitisha kwamba mazungumzo hayo yalifanyika kwa faragha.
Makamu wa rais wa pili Seif Ali Idd pia amedaiwa kuhudhuria mkutano huo kulingana na duru hizo.
Bw
Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kifupi kabla ya kuteuliwa
kuwania urais mwaka 1985 huku Karume akiliongoza eneo hilo kutoka mwaka
2000 hadi mwaka 2010.
Maafisa wa ikulu ya rais visiwani Zanzibar hawakuwa tayari kuzungumzia kuhusu yalioafikiwa katika mkutano huo.
Wale kutoka CUF hata hivyo wamesema kuwa majadiliano yalikuwa mazuri kwa maslahi ya raia wa muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment