Monday, 9 November 2015

Rais wa Nigeria afukuza kazi mwingine.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amemfukuza kazi mkuu wa Taasisi ya kupambana na Rushwa nchini humo.
Hata hivyo bado hazijatajwa sababu zilizofanya kuondolewa katika nafasi hiyo.
Rais Buhari alishinda kiti cha Urais nchini humo, katika uchaguzi uliofanyika mwaka huu.
Zaidi ya miezi mitano baada ya kuingia madarakani, baraza lake jipya la mawaziri linatarajiwa kuapishwa baadaye wiki.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema Rais Buhari anataka kuhakikisha kwamba mawaziri wapya atakao wateua hawatatumia ofisi kwa faida zao binafsi.

No comments:

Post a Comment