KUKUA KWA UCHUMI WA TANZANIA


Waziri wa Fedha asisitizia usimamizi wa mikakati iliyowekwa Waziri wa fedha Saada Mkuya amesema uchumi utaweza kukua na kuiwezesha Tanzania kufikia katika nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 endapo mikakati mbalimbali ya ukuaji wa uchumi iliyowekwa itasimamiwa ipasavyo ikiwemo ukamilishaji wa utekelezaji wa MKUKUTA Awamu ya pili pamoja na mpango wa maendeleo wa miaka 5.
Waziri Mkuya ametoa kauli hiyo jijini dar es salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili iliyolenga kujadili namna ya kuweza kufikia kusimamia matokeo katika kujenga uwezo kwenye masuala ya utengamano wa kikanda, Licha ya Tanzania kutokuwa mwanachama wa COMESA imehusishwa katika utekelezaji wa mpango ujulikanao AFRIC4R kutokana na juhudi zake.
Aidha Waziri Mkuya amesema mpango huu utawezesha Tanzania kujitambua iko katika nafasi gani katika kutokomeza umasikini ambao unapungua kwa kasi ndogo ya asilimia 2 ukilinganisha na kasi ya ukuaji wa uchumi ambayo ni asilimia 7 kwa mwaka
Washiriki wa warsha hiyo watakubaliana mwongozo utakaotumika katika michakato mbalimbali ikiwemo ukuaji wa uchumi, kupunguza umasikini na kujenga uwezo wa wananchi katika utendaji kazi kila siku
No comments:
Post a Comment