KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI ZA JUU MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ESALAAM
Gwaride
la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la
Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama
wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga
Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha
Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa
Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya
Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la
uvishaji cheo.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa
maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya
kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya
Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment