
Ripoti kutoka Orlando Marekani
zasema Omar Mateen, mtu aliyewafyatulia risasi na kuwaua watu 49 katika
klabu moja ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, alikuwa
akitembelea klabu hiyo iitwayo Pulse mara kwa mara.
Wahudumu na
meneja wa klabu hiyo amenukuliwa na magazeti ya Marekani akisema kuwa,
ameshawahi kumuona Mateen, hata akinywa pombe katika eneo hilo.
Naye
mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu aliyekuwa
na tabia za ugomvi wa mara kwa mara na kutaka kupigana na watu na wala
hakuwa na itikadi kali za kidini.
Mke huyo pia anaongeza kusema kuwa, wakati mwengine alionekana kutokuwa na akili timamu.
Baadhi ya wateja wa klabu hiyo wanasema kwamba, alikuwa katika mtandao wa watu wa wapenzi wa jinsia moja.
Waandishi
wa habari nao wanasema kuwa, taarifa zinazofichua alivyokuwa Mateen,
zinaibua maswali chungu nzima kuhusiana na kiini cha shambulizi hilo,
ambapo mshambuliaji anadi kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi la Islamic
State.
No comments:
Post a Comment