Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema mustakbali wa Ulaya
unategemea matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza kama itasalia au
itatoka katika Umoja wa ulaya. Rais Hollande amesema hayo baada ya
mazungumzo pamoja na waziri mkuu wa Slovakia Robert Fico, mnamo mkesha
wa kura ya maoni ambapo Waingereza watachagua kama wanataka nchi yao
itoke au Brexit au isalie katika Umoja wa ulaya. Rais Hollande anasema
Paris itauangalia uamuzi wa waingereza kuwa "usiobadilishika" na
kuongeza "London itakumbwa na hatari kubwa ikiwa haitokuwa na njia ya
kuingia katika soko la pamoja. Rais Francois Hollande wa Ufaransa
alikuwa kila mara akiitetea umuhimu wa Uingereza kusalia katika Umoja wa
Ulaya. Wito kama huo umetolewa pia na kansela Angela Merkel wa
Ujerumani hii leo. "Bila ya shaka ninataka Uingereza iendelee kuwa
mwanachama wa Umoja wa ulaya lakini uamuzi wanao wananchi wa Uingereza"
amesema Kansela Merkel mbele ya maripota baada ya mazungumzo pamoja na
Waziri Mkuu wa Poland, Beata Szydlo
No comments:
Post a Comment