Kilimo cha zao la Alizeti: Masoko, Mbinu na Ushauri toka kwa wadau
Nimekuwa navutiwa sana na ukulima wa alizeti kama zao la biashara. Naomba mawazo ya mdau yeyote mwenye uzoefu na kilimo hiki na namna gani unaweza kupata faida; Masoko yanapatikanaje na pia je ni faida zaidi kulima alizeti na kuuza ama kulima na kukamua mafuta? Naleta hoja.
Ni kweli mheshimiwa Kapuku: tarehe ya kupanda lazima ujue alizeti yako huchukua siku ngapi hadi kuvuna ili upande iweze kukomaa wakati kipindi cha mvua kimeshaisha. Alizeti ikikomaa huku mvua bado inanyesha vichwa vyake huoza.
Kuna imani kwamba alizeti iliyochelewa kupandwa huwa na mafuta mengi! Yawezekana ikawa na mafuta mengi kwa gunia moja lakini mavuno kwa shamba zima yakawa kidogo kiasi kwamba wingi wa mafuta kwenye hayo mavuno kidogo hauwezi kuzidi alizeti yenye mafuta kiasi lakini yenye mavuno makubwa.
Pamoja na kwamba alizeti inastahimili ukame lakini inahitaji mvua za kutosha pale zinapoweza kupatikana! Cha kuepuka ni isije ikakomaa huku mvua bado zinaendelea! Morogoro Mvua za kupandia alizeti ni za mwezi February mwishoni na mwezi wa March mwanzoni! Ukitaka alizeti yenye mafuta mengi panda mwezi wa April lakini utapata mavuno kidogo! Alizeti iliyositawi wastani wa mavuno ni magunia 15 ingawa wakulima wengi wanaishia gunia 8 hadi 10 tu kwa ekari moja.
Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro walishaachana na mbegu ya aina ya Record siku nyingi, kuna alizeti fupi toka Kenya zinazaa sana na zina mafuta mengi. Pia kuna alizeti Hybrid nazo ni fupi na mambo yake ni makubwa! Kama umepania kujichimbia kwenye kilimo cha alizeti anzia na Record lakini ukipata fursa ya kuwasiliana na mikoa ya Kaskazini ulizia mbegu za kutoka Kenya utaona vitu vyake! Tanzania utafiti wetu unasua sua sana kiasi kwamba toka iwepo mbegu ya Record hawajatoa mbegu nyingine, Record imepitwa na muda, haina mavuno makubwa wala haina mafuta mengi kama mbegu maarufu ambazo zinapatikana mikoa ya Kaskazini!
Pia lazima ikumbukwe kuwa alizeti hukubali sana inapowekewa mbolea za kukuzia (Nitrogen) kama Urea, CAN, SA nk kulingana na aina yako ya udongo. Kwa hiyo kama ikitokea unaona zao lako halieleweki ujue rutuba haitoshi! Hebu fanya jaribio kidogo sehemu ndogo weka mbolea uone matokeo yake! Nchi zilizoendelea hawalimi mazao haya bila mbolea ili wapate kipato kikubwa! Pamoja na imani kwamba Morogoro ni nchi yenye rutuba zipo sehemu zingine ni choka mbaya tu unakuta mtu anavuna vichwa vya alizeti kama kichwa cha tochi ya Tiger mwee!! Wekeni mbolea!!
No comments:
Post a Comment