Jeshi la Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bundeswehr,
litakuwa siku za mbele linalinda sio tu mwambao wa Libya, bali pia
kuwaandama wafanyabiashara haramu wa silaha. Baraza la mawaziri
limekubaliana operesheni ya ukaguzi wa manuari za Umoja wa Ulaya katika
Bahari ya Mediterenia, inayojulikana kwa jina la Sophia, ipanuliwe.
Juhudi za kusimamia utekelezaji wa vikwazo vya silaha vilivyowekwa na
Umoja wa Mataifa zimelengwa kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali wa Dola
la Kiislam wasipatiwe silaha katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.
Zaidi ya hayo, kwa kupanuliwa shughuli za ukaguzi za manuari za Umoja wa
Ulaya, itapatikana njia pia ya kupatiwa mafunzo walinzi wa fukwe za
Libya. Uamuzi wa baraza la mawaziri unabidi uidhinishwe na bunge la
shirikisho, Bundestag. Hata hivyo, serikali kuu ya muungano inadhibiti
wingi wa viti bungeni.
No comments:
Post a Comment