Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENCHI
la Ufundi la Kikosi cha Yanga limeweka wazi kuwa hali ya beki wake wa
kushoto Oscar Joshua aliyeumia katika mchezo wa kwanza wa kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia anaendelea vizuri na atarejea
uwanjani tena Jumanne kukipiga na TP Mazembe huku beki wa kulia Juma
Abdul anaendelea vizuri na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mepesi.
Abdul
alikosa mechi ya awali baada ya kuwa majeruhi kwa kuumia sehemu ya
kifundo cha mguu na kuukosa mchezo wa kwanza na nafasi yake ikichukuliwa
na Mbuyi Twite. Hata hivyo kwa sasa anaendelea vizuri na daktari
ameweka wazi kuwa anaweza kuanza mazoezi na timu itakaporejea ataungana
na wenzake.
Mkuu
wa Kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro (Pichani)amesema kuwa
Joshua anaendelwa vizuri na watakaoukosa mchezo huo ni Beki wa kushoto
Mwinyi Haji aliyepata kadi nyekundu pamoja na mshambuliaji Amisi Tambwe
mwenye kadi mbili za njano alizozipata kwenye mchezo wa marudiano na
Segrada Esperanca ya Angola na wa hatua ya makundi na Mo Bejaia.
"Ni
wachezaji wawili tu ndiyo watakaokosa mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao
ni Mwinyi anayetumikia kadi nyekundu na Tambwe mwenye kadi mbili za
njano, kwahiyo katika mchezo huo Oscar atarejea tena uwanjani na Abdul
anaendelea vizuri ameanza mazoezi mepesi mepesi na pindi timu
itakaporejea ataungana nao,"amesema Muro.
Kwa
sasa Yanga inaendelea na mazoezi katika jiji la Antalya nchini Uturuki
ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao utapigigwa Siku ya
Jumanne Juni 28 na unatarajiwa kuwa wa ushindani wa hali ya juu hasa
baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa awali na wakihitaji matokeo na TP
Mazembe wakitaka ushindi ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kuingia nusu
fainali.
No comments:
Post a Comment