Moise Katumbi ahukumiwa miaka 3 jela

Mgombea urais wa
upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa
kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye
mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya dola milioni 6.
Katumbi
hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri
kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali
kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.
Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi
amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha
kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba
No comments:
Post a Comment