Eritrea na Ethiopia zimetupiana lawama kwa kuanzisha mapigano mwishoni
mwa juma baina ya majeshi yake katika eneo la mpakani linalotumiwa na
nchi zote mbili la Tsorona.
Eritrea na Ethiopia zimetupiana lawama kwa kuanzisha mapigano mwishoni
mwa juma baina ya majeshi yake katika eneo la mpakani linalotumiwa na
nchi zote mbili la Tsorona, ikiashiria kuendelea kwa mgogoro wa mpaka
uliochochea vita baina ya mataifa hayo mawili mwaka 1998 hadi 2000.
Ethiopia imesema kwamba hali ilitulia hapo jana, baada ya wakaazi
wanaoishi upande wa nchi hiyo kutoa taarifa za kusikika kwa milipuko
iliyodumu siku nzima ya Jumapili hadi Jumatatu asubuhi.
Eritrea nchi iliyo Pembe ya Afrika, ilijipatia uhuru kutoka mikononi mwa
Ethiopia mnamo mwaka 1991. Takribani watu 70,000 waliuawa katika vita
ya kugombea mpaka baina ya mataifa hayo mawili.
Waziri wa habari wa Eritrea amesema kwamba serikali ya Ethiopia
ilianzisha mashambulizi dhidi ya nchi yake katika eneo la mbele la
Tsorona.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini New
York kuwa katibu mkuu Ban Ki-moon anao wasiwasi juu ya mapigano hayo na
tayari anataka kuzifikia pande zote mbili.
Amesema kwamba "katibu mkuu anazitaka serikali zote kujizuia na kufanyia
kazi utatuzi wa tofauti zao kwa njia ya amani, ikiwemo utekelezaji wa
makubaliano ya amani waliyosaini mwaka 2000" amesema waziri huyo.
Umoja wa Mataifa ulipeleka kikosi cha kufuatilia makubaliano ya
kusitishwa kwa mapigano mwaka 2000 katika mpaka baina ya nchi hizo
mbili , lakini hata hivyo ilikiondoa kikosi hicho 2008 kutokana na
vikwazo vilivyowekwa na Eritrea na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa
ujumbe huo.
Ethiopia kwa upande wake nayo imekanusha kuanzisha chokochoko ikisema kwamba ni majeshi ya Eritrea yaliyoanzisha fujo hizo.
Waziri wa habari wa Eritrea Yemene Ghebremeskel hakuwa na maoni juu ya
majeruhi au taarifa nyingine juu ya mashambulizi hayo.Maafisa wa
Ethiopia nao hawajatoa taarifa ikiwa kulikuwa na majeruhi.
Umoja wa Mataifa unaishutumu Eritrea kwa ukiukwaji wa muda mrefu wa haki
za huduma za kitaifa ambapo raia wa nchi hiyo hutumia muda mrefu
wakilipwa ujira mdogo kwa mujibu wa sheria.
Charlotte King, mchambuzi mwandamizi wa Afrika katika kitengo cha
intelijensia ya uchumi anasema wakosoaji wa Eritrea wataona kama nchi
hiyo inajaribu kukwepa tahadhari ya jumuiya za kimataifa dhidi ya
uhalifu wa ubinaadamu na kuhalalisha mahitaji yake ya kijeshi.
Eritrea iliyo na vikwazo vya Umoja wa mataifa inasema mataigfa yenye
nguvu yameshindwa kuishinkiza Ethiopia kukubaliana na usuluhishi wa
kimataifa unaotawala mpaka huo. Ethiopia imesema inataka mazungumzo kwa
ajili ya utekelezaji.
No comments:
Post a Comment