Timu ya Algeria kuwasili kesho

Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria unatarajiwa kuwasili Tanzania kesho kwa ndege binafsi ya kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65.
Msafara
huo utajumuisha wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14
dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha
mkuu wa timu hiyo Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi
cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya
kwa ajili ya kuikabili Tanzania.
Mchezo huu wa raundi ya pili ni
wa kuwania kuingia katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kombe la
dunia litakalofanyika huko nchi Urusi mwaka 2018
No comments:
Post a Comment