Profesa Muhongo aelezea mikakati Sekta za Nishati na Madini, Benki ya Dunia yafurahishwa na utekelezaji wake
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongoza kikao
kilichoshirikisha Watendaji kutoka Benki ya Dunia pamoja na watendaji
kutoka Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake ikiwa ni pamoja
na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa
Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA).
Mtendaji
Kutoka Benki ya Dunia anayeshughulikia mazingira Vladislav Vucetic,
akielezea mikakati ya benki hiyo katika ushirikiano wake na Serikali
ili kupanua sekta za nishati na madini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto
waliokaa mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Juliana Pallangyo ( wa pili
kutoka kushoto waliokaa mbele) wakifuatilia kwa makini maelekezo
yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo( hayupo pichani) katika kikao hicho.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameelezea mikakati ya
Serikali katika uboreshaji wa sekta za nishati na madini na kuongeza
kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na Benki ya Dunia (WB)
katika uboreshaji wa sekta hizo ili ziwe na mchango mkubwa katika
ukuaji wa uchumi wa nchi.
Profesa
Muhongo aliyasema hayo alipokutana na Watendaji kutoka Benki ya Dunia
pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na taasisi
zake ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini
(TPDC) na Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA)
No comments:
Post a Comment