
Nyota wa Sweden Zlatan Ibrahimovich ametangaza kwamba atastaafu katika soka ya kimataifa baada ya michuano ya Euro 2016.
Taifa
lake linakutana na Ubelgiji katika mechi ya mwisho ya kundi E siku ya
jumatanoambayo huenda ikawa mechi yake ya mwisho kwa taifa lake.
Alisema:Ninajivunia kile nilichofanikiwa kupata na kila mara nitatembea na bendera ya Sweden.
Klabu
ya Manchester United imehusishwa pakubwa na mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 34 ambaye alikuwa ajenti huru baada ya kuondoka klabu ya Paris
Saint Germain ya Ufaransa .
No comments:
Post a Comment