MAKALA YA AMINA CHIFUPA NA HISTORIA YA KUSIKITISHA PAMOJA NA KIFO CHAKE
Marehemu mpiganaji Amina Chifupa.
- Alifariki akiwa na umri wa miaka 26 tarehe 26 siku ya dunia kupiga vita dawa za kulevya
- Alikuwa mwanaharakati wa kupinga biashara ya dawa za kulevya
Leo nimeona nijitokeze kuandika makala haya kupitia mtandao huu wa kijamii wa www.vitalisymalata.blogspot.com Makala ambayo ni Mbegu kwa waandishi wengine.
IKUMBUKWE
kuwa Juni 26, 2007 ilikuwa ni siku ya Jumanne ambayo kwa watunza
kumbukumbu za matukio yanayogusa jamii ni siku ambayo haitosahaulika
kirahisi nchini Tanzania kufuatia Taaarifa za kushtua, baada ya Mbunge
wa Viti Maalum, Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Amina
Chifupa Mpakanjia kufariki dunia.
Amina Chifupa alifariki akiwa na umri wa
miaka 26 majira ya saa 3:00 katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi
(JWTZ) Lugalo Dar es Salaam kwa maradhi ya mfadhaiko wa akili yaani
“depression”.
Majuma mawili kabla ya kifo chake Spika wa
bunge la 9 Samuel Sitta aliwatangazia wabunge kuhusu kuugua kwa Amina
na akawaomba wabunge wamwombee aweze kupona haraka, hata mbunge wa
jimbo la Mbinga Magharibi alipopata nafasi ya kuchangia hotuba ya bajeti
ya Waziri Mkuu wa 2007/08 aliwasihi wabunge waendelee kumwombea Amina
ili aweze kupona.
Kuugua kwa Amina kulianza kama mzaha huku kukigubikwa na habari za yeye kutalakiwa na mumewe Mpakanjia.
Ilidaiwa kwamba Mpakanjia alimtariki Amina
baada ya kuwapo kwa habari kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA) hali iliyowafanya wachunguzi
wa mambo kuamini kuwa ndiko kulikomsababishia ugonjwa wa mfadhaiko wa
akili.
Taarifa
za madaktari wa Lugalo zilionyesha kuwa Amina alifariki kutokana na
shinikizo la damu na kisukari, magonjwa ambayo haikuwahi kushuhudia
wakati wa uhai wake.
Wengine wanadai kilichomuua Amina, mmoja ni kujitoa kwake mhanga katika vita dhidi ya mihadarati kwa maana ya dawa za kulevya.
Kwa ufupi ni mbunge ambaye alisimama kidete
kutoboa siri za biashara za mihadarati na kuna wakati alipata
kutishiwa na Polisi na kulazimika kumpa ulinzi kwa muda kutokana na
vitisho hivyo.
Amina alifariki akiwa na
msuguano na baadhi ya viongozi wa UVCCM ambao walituhumiwa kumwona
kuwa tishio katika nafasi ya uenyekiti wa Umoja huo ngazi ya Taifa.
Amina alizaliwa Mei 20, 1981 mjini Dar es
Salaam, alisoma Shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni Dar (1988-1994) kabla
ya kujiunga na masomo ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha nne
katika Shule ya Wasichana ya Kisutu, Dar (1995-1998). Elimu ya Juu ya
Sekondari alisoma katika shule ya Makongo (1999-2001) kabla ya kujiunga
na Chuo cha Uandishi wa Habri cha Royal (2001-2003) ambako alifuzu
Diploma ya Uandishi wa Habari.
Mwaka 1999 alianza kazi ya Utangazaji wa
Kituo cha Redio cha Clouds FM cha Dar na aliwahi kuwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mama Shughuli.
Katika CCM aliwahi kuwa Kamanda wa CCM wa
umoja wa Vijana katika tawi la Mikocheni A jijini Dar na amekuwa Katibu
wa Kamati ya Uchumi ya UVCCM mkoa wa Dar, aliwahi kuwa Mama Mlezi wa
UVCCM na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) matawi ya Bunju na Mbagala.
MAZISHI YAKE
Maelfu
ya wakazi wa Jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake siku ya Jumatano
ya Juni 27, 2007 walifurika pembezoni mwa barabara za Bagamoyo na
Kambarage wakiwa wameduwaa, wenye majonzi wakiupokea mwili wa aliyekuwa
Mbunge wa Viti Maalum CCM Amina Chifupa.
Mwili wake uliwasili nyumbani kwao Mkocheni
saa 7:58 mchanaukiwa katika jeneza lililopambwa kitambaa
kilichodariziwa na nakshi zenye rangi ya dhahabu ukitokea katika
hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam.
Mara
baada ya kuwasili nyumbani hapo Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Shaban
Simba aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika sala maalumu ya kumwombea
marehemu na baadaye mwili huo ukaingizwa ndani ambako ulipokelewa kwa
vilio vya nguvu kutoka kwa watu waliohudhuria.
Katika msiba huo siku hiyo wengi
waliufananisha na msiba wa aliyekuwa mke wa watoto wa Malkia wa
Uingereza, Marehemu Princess Diana au ule wa Waziri Mkuu Edward Moringe
Sokoine.

Nyumbani kwa mzee Khamis Chifupa, baba
mzazi wa Amina watu walikuwa wamefurika licha ya ukubwa wa eneo la
makazi hayo na hivyo kusababisha msongano.
Hali hiyo ilisababisha Meya Manispaa ya
Kinondoni wakati huo Salum Londa kuingilia kati na kusaidia kamati ya
mazishi kuwapanga na kuwatuliza waombolezaji.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam
wakati huo Hemed Mkali alisema kuwa kifo cha Amina kimedhihirisha kuwa
kweli alikuwa anaumizwa na matatizo ya dawa za kulevya nchini kwani
kimetokea siku iliyotengwa na dunia kupiga vita dawa za kulevya.
Meya wa Jiji la Dar wakati huo Adama
Kimbisa alisema Amina alikuwa kijana mwenye kusimamia ukweli, haki na
maadili. Kimbisa alisema katika vikao mbalimbali jambo na kulitetea kwa
kufuata misingi ya haki.
Mkurugenzi wa Clouds FM Joseph Kusaga
alimwelezea Amina Chifupa ilikuwa ni hazina kwa taifa hasa kwa wasichana
wadogo kutokana na kipaji alichojaliwa kujiamini katika maisha yake
tangu utotoni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) wakati huo Profesa Mark Mwandosya alisema kifo cha Amina
kimeacha changamoto kubwa kwa serikali na wadau wengine kushughulikia
tatizo la kushamiri kwa dawa kulevya nchini.
Kwa upande wake Maalim Seif Shariff Hamad
Katibu Mkuu wa CUF alisema Amina alishughulikia kero mbalimbali
zinazoiathiri jamii bila kujali itikadi za kisiasa, alikuwa mwanasiasa
chipukizi aliyejitolea kushughulikia kero za wananchi bila woga.
Tutamkumbuka kwa ucheshi na uwezo mkubwa wa kujenga hoja mbalimbali ndani na nje ya Bunge. Katika kipindi kifupi akiwa Mwanasiasa kijana, aliweza kusimama na kujipembua na wabunge wengine kwa kusimama kidete kupiga vita biashara ya mihadarati ambayo alaiamini inaua vijana ambao ni viongozi wa kesho.
Alipata Ubunge Desemba 28, 2005 akitakiwa
kudumu katika bunge kwa miaka mitano hadi Desemba 27, 2010. Namba yake
ya Usajili kama Mbunge ilikuwa ni 1313.
Alizikwa majira ya saa 10 jioni ya Juni 28,
2007 kijijini Lupembe Wilayani Njombe mkoa wa Iringa wakati huo,
karibu kabisa na eneo alilokuwa akiishi bibi yake.
No comments:
Post a Comment