Tuesday, 10 November 2015

Suu Kyi asema uchaguzi ulikuwa wa haki

Kiongozi wa upinzani Myanmar Aung San Suu Kyi ameambia BBC kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki.
Kwenye mahojiano ya kipekee, Bi Suu Kyi aliwapongeza watu wa Myanmar. Matokeo ya mapema yanaonyesha chama chake cha National League for Democracy (NLD) kitapata ushindi mkubwa.
Chini ya katiba ya chini hiyo hawezi akawa rais, lakini amesema kwamba kama kiongozi wa chama atamteua rais.
Uchaguz huo umechukuliwa na wengi kuwa ulio wa kidemokrasia zaidi katika miaka 25, baada ya miongo kadha ya uongozi wa kijeshi.
Matokeo rasmi ya uchaguzi yalianza kutolewa Jumatatu, lakini matokeo kamili yanatarajiwa kuchukua siku kadha.
Chama cha NLD kimeshinda viti vingi vya ubunge kati ya vile ambavyo matokeo yake yametangazwa.
Chama tawala cha Union Solidarity Development Party (USDP) kinachoungwa mkono na jeshi, kimekuwa madarakani tangu 2011 taifa hilo lilipoanza shughuli ya mpito kutoka utawala wa kijeshi hadi uongozi wa kiraia.
Alipoulizwa iwapo uchaguzi huo huenda ukahujumiwa, Bi Suu Kyi alijibu kwamba watakaofanya hivyo watakuwa wanahujumu mapenzi ya raia

No comments:

Post a Comment