MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YAFANA SANA JIJINI MONTREAL, CANADA
Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Utalii ambayo yamedumu kwa siku tatu mfululizo katika jiji la Montreal nchini Canada yafana
sana. Ubalozi wa Tanzania, Ottawa nchini Canada ulikuwa ni mmoja wa
washiriki kati ya washiriki waonyeshaji 400 walioalikwa na sekta ya
utalii ambayo ndiyo muandaaji rasmi wa maonesho hayo.
Maonyesho
hayo ambayo yamefanyika katika mahali maarufu la “la Place
Bonaventure” katika jiji la hilo, ambalo liko upande wa Mashariki mwa
Canada, eneo ambalo wengi wa wakazi wake huzungumza Kifaransa, yamekuwa
na hamasa na mashiko makubwa mwaka huu kwa kupata wahudhuriaji zaidi ya
elfu thelathini na tatu (33,000).
Kutokana
na wingi wa watu, wakiwemo watalii wanaopenda kuzuru nchi mbalimbali,
waliohamasika kuhudhuria maonesho hayo, Balozi wa Tanzania Mhe. Jack
Mugendi Zoka aliamua kuwa kati ya waonyeshaji na watoa taarifa za
vivutio vya utalii katika banda lake kama ionekanavyo katika picha hapo
chini.
Aidha,
mabalozi wa nchi mbalimbali walifika katika banda la utalii la Tanzania
kujionea ni jinsi gani limeweza kuwa kivutio cha watalii wengi. Balozi
wa nchi jirani ya Kenya alikuwa miongoni mwa watembeleaji katika banda
hilo.
No comments:
Post a Comment