Mabalozi waonya maafisa wafisadi Kenya

Mabalozi hao wameitaka serikali ya Kenya isaidie tume ya kupambana na rushwa
Mabalozi wa mataifa
ya kigeni wameonya kuwa huenda mataifa yao yakawapiga marufuku maafisa
wa serikali wanaojihusisha na ufisadi kuzuru nchi hizo.
Kupitia
taarifa ya pamoja, mabalozi hao kutoka mataifa 11 wameahidi kusaidia
katika uchunguzi dhidi ya maafisa wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi.
Aidha, wameahidi kusaidia kutwaa mali na pesa zilizofichwa nje ya nchi na maafisa wafisadi.
Taarifa
hiyo imetolewa baada ya mkutano wa faraghani kati ya mabalozi hao na
wakuu wa tume ya maadili na kupambana na rushwa Kenya, EACC.
Mabalozi
hao, waliojumuisha balozi wa Marekani Robert Godec na mwenzake wa
Uingereza Christian Turner, pia wameitaka serikali kuisaidia tume ya
EACC kutekeleza majukumu yake.
Taarifa yao imetokea wakati ambapo visa vya ufisadi serikali vimekuwa vikiripotiwa sana katika vyombo vya habari.
Wakuu
wa wizara za serikali zilizotajwa kwenye tuhuma hizo, wakiwemo Waziri
wa Usalama Joseph Nkaissery na Waziri wa Mipango Anne Waiguru,
wamekanusha tuhuma hizo.
Mabalozi wengine waliohudhuria kikao cha
leo ni Jamie Christoff (Canada), Tarja Fernández (Finland), Remi
Marechaux (Ufaranca), Jutta Frasch (Ujerumani), Mikio Mori (naibu
balozi, Japan), Marielle Geraedts (naibu balozi, Uholanzi), Victor
Rønneberg (Norway), Johan Borgstam (Sweden) na Ralf Heckner (Uswisi).
No comments:
Post a Comment