Marekani yaahidi zawadi kwa habari kuhusu al-Shabab
Marekani imeahidi $6 milioni kwa habari kuhusu aliko kiongozi wa al-Shabab
Marekani imehaidi
kutoa zawadi ya jumla ya $27 milioni kwa yeyote atakayetoa habari
zitakazowezesha kukamatwa kwa viongozi sita wakuu wa kundi la al-Shabab.
Wizara
ya mashauri ya kigeni ya Marekani imetangaza kuwa Marekani itatoa $6
milioni kwa habari kumhusu Abu Ubaidah (Direye), $5 milioni kwa habari
kuhusu kila mmoja kati ya Mahad Karate, Ma’alim Daud, na Hassan Afgooye,
na $3 milioni kwa habari za kila mmoja kati ya Maalim Salman na Ahmed
Iman Ali.
Viongozi hao wa kundi hilo la Somalia wanasakwa kwa
kupanga mashambulio ya kigaidi likiwemo shambulio la Chuo Kikuu cha
Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya mwezi Aprili.
Marekani
imesema sita hao wamekuwa wakihusika katika kufadhili, kusajili
wanachama na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa al-Shabaab.
Bw
Ubaidah alifanywa kiongozi wa al-Shabaab mwaka jana baada ya mtangulizi
wake Ahmed Godane kuuawa kwenye shambulio la ndege za Marekani.
Ubaidah
amesisitiza kwamba kundi hilo bado ni tiifu kwa Al Qaeda, ingawa majuzi
kuna kundi la wapiganaji hao lililojiunga na Islamic State
No comments:
Post a Comment