hatimaye historia ya Mzee Rashid Kawawa yaandikwa... Kikwete azindua kitabu.. akoromea wanaojidai wanajua kumbe wanatanga na jua
RAIS
Jakaya Kikwete amewaonya baadhi ya viongozi wa serikali wastaafu
wanaokwamisha utendaji wa serikali iliyopo madarakani kwa kutoa kauli
vijiweni zinazoashiria kuwa imeshindwa kiutendaji huku wakisahau kuwa
wanayoyasema hawakuyafanyia kazi kipindi cha uongozi wao.
Aidha ameonya tabia hiyo na kuwakumbusha viongozi hao kutambua kuwa kipindi chao cha kuwa madarakani kimekwisha na kazi kubwa walionayo ni kutoa ushauri kwa walioko madarakani badala ya kuwa vikwazo katika juhudi zao za kuleta maendeleo.
Rais aliyasema hayo leo, Ikulu, Dar es Salaam wakati akitoa hotuba mara baada ya kuzindua kitabu cha historia ya Rashid Mfaume Kawawa kiitwacho ‘Simba wa Vita katika Historia ya Tanzania, Rashid Mfaume Kawawa’ kilichoandikwa na Dk. John Magotti.
Magotti ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigambo, Dar es Salaam na amefanya kazi na Kawawa kwa muda mrefu.
Katika hafla hiyo iliyohusisha pia sherehe za kuzaliwa kwa Kawawa aliyetimiza miaka 83 leo na, viongozi wastaafu na walioko madarakani waliyohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Marais Wastaafu, Ali Hassan Mwingi na Benjamin Mkapa, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Jaji Joseph Warioba na John Malecela.
Wengine ni Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Bara), George Kahama, Mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere, Kingunge Ngombale Mwiru, viongozi wa taasisi za serikali na zisizo za serikali, Mashirika ya Kimataifa pamoja na familia ya Kawawa.
Kikwete akitoea mfano unyenyekevu wa Kawawa katika kipindi chote akiwa kiongozi katika ngazi mbalimbali nchini, alisema viongozi wengine wanakosa kufahamu kuwa kila jambo lina wakati wake hivyo wanajikuta wakitoa kauli za vijiweni zinazokwamisha maendeleo.
“Nakushuru Mzee Kawawa kwa kipindi chote cha kupanda na kushuka kwa uongozi wako hukuwa kama baadhi ya viongozi wengine wanaosahau wajibu wao wa kuwasaidia walioko madarakani na kujikuta wanapiga maneno vijiweni yasio mazuri,” alisema Kikwete na kuongeza;
“Inashangaza mtu huyo enzi za kuwa madarakani yeye hayo hakuyaona na wala kuyafanya…….., wewe siku zote umekuwa ukishauri pale unapoona mambo hayaendi sawa na tunakushuru sana Mzee wetu Kawawa.

No comments:
Post a Comment