UN yawazia kutuma walinda amani Burundi

Raia wanaendelea kutoroka mitaa mingi Bujumbura
Umoja wa Mataifa unatafakari wazo la kutuma walinda amani nchini Burundi iwapo machafuko nchini humo yatazidi.
Watu
zaidi ya 200 tayari wameuawa na maelfu wengine kutoroka makwao tangu
Aprili, Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba angewania urais wka
muhula wa tatu.
Mnamo Jumatano, Rais Nkurunziza alipuuzilia mbali
madai kwamba huenda kukatokea mauaji ya kimbari nchini humo na
akawahimiza Warundi waungane.
Mwandishi wa BBC anayeangazia
masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo anasema Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa litapiga kura baadaye Alhamisi kuidhinisha azimio la
kukashifu machafuko Burundi.
Kadhalika, mabalozi wanaowakilisha
nchi mbalimbali wanatarajiwa kutoa wito kwa UN na mataifa ya kanda ya
Afrika Mashariki kuchukua hatua.
Muungano wa Afrika tayari
umekitaka kikosi cha polisi wa akiba cha kanda ya Afrika Mashariki kuwa
tayari kutumwa Burundi iwapo hali itakuwa mbaya zaidi.
Hata hivyo, uamuzi wa kutuma wanajeshi nchini Burundi unafaa kufanywa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Milio ya risasi bado imekuwa ikisikika katika mitaa ya mji mkuu Bujumbura, huku raia wakishambuliwa mara kwa mara.
Nahodha
wa timu ya kandanda ya rais Nkurunziza aliyetambuliwa kwa jina Jamal
mwenyewe alinusurika kifo baada ya kupigwa risasi mara kadha miguuni
Jumatano usiku.
Visa kama hivyo vinaipa serikali sababu zaidi za kuendelea na operesheni ya kusaka silaha katika ngome za wapinzani.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanasema serikali inaangazia tu wapinzani lakini haiangazii vitendo vya wanajeshi wake
No comments:
Post a Comment