Thursday, 12 November 2015


JUMUIYA YA ULAYA (EU) YATOA EURO 200,000 KWA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI TANZANIA





Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa EU, Eric Beaume. (Picha na Francis Dande)

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA ya Ulaya (EU)imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), ruzuku Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478.



Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini , Alvaro Rodriguez na Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi.

Sebregondi alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.



Naye Rodriguez, alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU NA UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.

Rodriguez, alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya endelevu SDGs.

Mchezaji achunguzwa kwa kuchokoza mbwa

Oakland
Klabu ya mchezaji huyo ilishindwa kwenye mechi hiyo
 
Mchezaji wa Oakland Raiders Ray-Ray Armstrong anachunguzwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za ‘kubweka’ na kujipiga kifua mbele ya mbwa wa polisi.
Armstrong, 24, anadaiwa kuinua shati lake na kumchokoza mbwa huyo kabla ya mechi ya NFL dhidi ya Pittsburgh Steelers Jumapili.
Akipatikana na hatia, huenda akashtakiwa na kosa la kumchokoza mbwa wa polisi, ambalo ni kosa la ngazi ya tatu jimbo la Pennsylvania.
"Mbwa huyo alijawa na hasira sana,” afisa mmoja wa polisi Kevin Kraus amesema.
"Afisa huyo alitatizika sana kumdhibiti mbwa huyo. Tulifahamishwa mara moja kuhusu kisa hicho na mara moja tukaanzisha uchunguzi.”
Afisa wa polisi aliyekuwa na mbwa huyo, Bi Maria Watts, amemtambua Armstrong kuwa ndiye aliyehusika katika kisa hicho.
Ameambia runinga ya WTAE Pittsburgh kwamba maafisa wa polisi wamekasirishwa sana na kisa hicho.
Klabu zote mbili zimejulishwa kuhusu tukio hilo na NFL imeanzisha uchunguzi.
Oakland Raiders walilazwa 38-35 na Steelers

Mabalozi waonya maafisa wafisadi Kenya

  Kenya
Mabalozi hao wameitaka serikali ya Kenya isaidie tume ya kupambana na rushwa
Mabalozi wa mataifa ya kigeni wameonya kuwa huenda mataifa yao yakawapiga marufuku maafisa wa serikali wanaojihusisha na ufisadi kuzuru nchi hizo.
Kupitia taarifa ya pamoja, mabalozi hao kutoka mataifa 11 wameahidi kusaidia katika uchunguzi dhidi ya maafisa wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi.
Aidha, wameahidi kusaidia kutwaa mali na pesa zilizofichwa nje ya nchi na maafisa wafisadi.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya mkutano wa faraghani kati ya mabalozi hao na wakuu wa tume ya maadili na kupambana na rushwa Kenya, EACC.
Mabalozi hao, waliojumuisha balozi wa Marekani Robert Godec na mwenzake wa Uingereza Christian Turner, pia wameitaka serikali kuisaidia tume ya EACC kutekeleza majukumu yake.
Taarifa yao imetokea wakati ambapo visa vya ufisadi serikali vimekuwa vikiripotiwa sana katika vyombo vya habari.
Wakuu wa wizara za serikali zilizotajwa kwenye tuhuma hizo, wakiwemo Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery na Waziri wa Mipango Anne Waiguru, wamekanusha tuhuma hizo.
Mabalozi wengine waliohudhuria kikao cha leo ni Jamie Christoff (Canada), Tarja Fernández (Finland), Remi Marechaux (Ufaranca), Jutta Frasch (Ujerumani), Mikio Mori (naibu balozi, Japan), Marielle Geraedts (naibu balozi, Uholanzi), Victor Rønneberg (Norway), Johan Borgstam (Sweden) na Ralf Heckner (Uswisi).

 

Msaidizi wa Lowassa achunguzwa uraia wake

Edward Lowassa akifanya kampeni za uchaguzi wa urais uliokamilika nchini Tanzania
Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamesema kuwa wanamzuia msaidizi wa aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Edward Lowassa ili kuchunguzwa kuhusiana na uraia wake.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo,wamesema kuwa bwana Bashir Fenel Awale Ally ambaye amekuwa mtu muhimu katika kampeni za urais za bwana Lowassa atachunguzwa kuhusiana na stakhabadhi zinazotilia shaka kuhusu uraia wake.
Kamanda maalum wa polisi katika eneo la Dar es Salaam, Suleiman Kova amewaambia waandishi wa habari kwamba stakhabadhi alizokamatwa nazo zinatatiza kuhusiana na taifa analotoka.
Amesema kuwa wakati wa kukamatwa kwake mtu huyo alipatikana na cheti cha kuzaliwa kinachoonyesha kwamba alizaliwa tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969 mjini Dodoma.
Kulingana na afisa huyo mshukiwa huyo pia alipatikana na pasipoti iliotoka jijini nairobi na ambayo inayoonyesha kwamba alizaliwa mjini humo mnamo tarehe 11 mwezi Julai mwaka 1969,akiwa na jina la Bashir Fenal Abdi Ally Awadhi .
Mshukiwa huyo anayedaiwa kuwa mwanaharakati na mfuasi mkubwa wa chama cha upinzani Chadema alikamatwa nyumbani kwake huko Mikocheni.
Kova amesema kuwa kuna ishara kwamba mshukiwa huyo ni raia wa Kenya.
Ameongezea kuwa sheria za Tanzania haziruhusu mtu asiye raia wa taifa hilo kushiriki katika maswala ya kisiasa ikiwemo kushiriki katika kampeni na kupiga kura.

UN yawazia kutuma walinda amani Burundi

 
 Raia wanaendelea kutoroka mitaa mingi Bujumbura 
 
Umoja wa Mataifa unatafakari wazo la kutuma walinda amani nchini Burundi iwapo machafuko nchini humo yatazidi.
Watu zaidi ya 200 tayari wameuawa na maelfu wengine kutoroka makwao tangu Aprili, Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba angewania urais wka muhula wa tatu.
Mnamo Jumatano, Rais Nkurunziza alipuuzilia mbali madai kwamba huenda kukatokea mauaji ya kimbari nchini humo na akawahimiza Warundi waungane.
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo anasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litapiga kura baadaye Alhamisi kuidhinisha azimio la kukashifu machafuko Burundi.
Kadhalika, mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali wanatarajiwa kutoa wito kwa UN na mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki kuchukua hatua.
Muungano wa Afrika tayari umekitaka kikosi cha polisi wa akiba cha kanda ya Afrika Mashariki kuwa tayari kutumwa Burundi iwapo hali itakuwa mbaya zaidi.
Hata hivyo, uamuzi wa kutuma wanajeshi nchini Burundi unafaa kufanywa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Milio ya risasi bado imekuwa ikisikika katika mitaa ya mji mkuu Bujumbura, huku raia wakishambuliwa mara kwa mara.
Nahodha wa timu ya kandanda ya rais Nkurunziza aliyetambuliwa kwa jina Jamal mwenyewe alinusurika kifo baada ya kupigwa risasi mara kadha miguuni Jumatano usiku.
Visa kama hivyo vinaipa serikali sababu zaidi za kuendelea na operesheni ya kusaka silaha katika ngome za wapinzani.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanasema serikali inaangazia tu wapinzani lakini haiangazii vitendo vya wanajeshi wake
Jeshi la Kenya latuhumiwa Somalia




Jeshi la Kenya limetuhumiwa kujihusisha na biashara, badala ya kufanya kazi zinazowahusu nchini Somalia.


Taasisi ya Wanahabari Wanaopigania haki imelituhumu jeshi hilo kujiingiza katika masuala yanayowaletea faida.

Taasisi hiyo imewalaumu baadhi ya maofisa wa jeshi kushirikiana katika biashara haramu na wapiganaji wa Al Shabaab.

Sikiliza mahojiano ya David Wafula na Msemaji wa Jeshi la Kenya Kanali David Obonyo, ambaye anakanusha tuhuma hizo

Hazina ya $1.9bn kwa Afrika yaidhinishwa

 EU
 Mamia ya watu wamekuwa wakifariki baharini wakijaribu kufika Ulaya
Viongozi wa Muungano wa Ulaya na Afrika wametia saini makubaliano yanayotarajiwa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaofunga safari hatari ya kutaka kufika Ulaya.
Viongozi hao wa EU, kwenye mkutano Malta, wameidhinisha kuundwa kwa hazina ya $1.9 bilioni za kusaidia mataifa ya Afrika.
Baadaye, viongozi hao watafanya mkutano usio rasmi ambapo watajadili suala ya uhamiaji Ulaya, yakiwemo mataifa ya Balkan.
Muungano wa Ulaya unakadiria kwamba watu 3 milioni huenda wakafika Ulaya wakitafuta hifadhi au nafasi za kazi kufikia 2017.
Miongoni mwa mataifa yatakayofaidi kutokana na hazina hiyo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Djibouti, Somalia, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia

Wednesday, 11 November 2015


JESHI LA POLISI LAKAMATA SILAHA 8 NA RISASI 62




Na. Lilian Lundo - Maelezo

JESHI la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 7 wakiwa na silaha 8 na risasi 62 kwenye msako uliofanyika jijini Dar es salaam katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.




Akiongea na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amesema wahalifu walidhani kuwa Jeshi la Polisi limeweka nguvu katika uchaguzi mkuu na kusahau kufanya misako yake iliyokuwa ikifanya mara kwa mara kama moja ya majukumu yake.




“Ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi lilijipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani na misako mingine inaendelea kufanyika kama kawaida kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na mikoa ya jirani” Alisema kamanda Kova.




Kamanda Kova aliongezea kwa kusema kuwa, Jeshi la Polisi kanda maalum inashirikiana na mikoa ya jirani kuhakikisha kuwa watuhumiwa hao hawapati fursa ya kukwepa mkondo wa sheria.
Aidha alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni SMG moja (1), Bastola sita (6) na Mark 4 riffle moja (1) na risasi 62 ambapo mpaka sasa jumla ya majambazi 74 wamekamatwa ikiwa ni pamoja na silaha 51 na risasi 890 za silaha mbalimbali.




Kamanda Kova amezidi kufafanua kuwa kutakuwa na msako mwingine mkali kuelekea sikukuu za x-mass na mwaka mpya 2016, utakayofanyika katika mikoa ya kipolisi ya Ilala, Kinondoni na Temeke wakisaidiwa na vikosi maalum vilivyopo Kanda ya Dar es Salaam.
Msako huo utajikita katika kuwakamata majambazi, magaidi, wanaojihusisha na madawa ya kulevya, vibaka, wapiga debe, wanaouza pombe haramu, madanguru yote ambayo pia huhifadhi wahalifu.

Marekani yaahidi zawadi kwa habari kuhusu al-Shabab

 Al-Shabab

Marekani imeahidi $6 milioni kwa habari kuhusu aliko kiongozi wa al-Shabab
 
Marekani imehaidi kutoa zawadi ya jumla ya $27 milioni kwa yeyote atakayetoa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa viongozi sita wakuu wa kundi la al-Shabab.
Wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani imetangaza kuwa Marekani itatoa $6 milioni kwa habari kumhusu Abu Ubaidah (Direye), $5 milioni kwa habari kuhusu kila mmoja kati ya Mahad Karate, Ma’alim Daud, na Hassan Afgooye, na $3 milioni kwa habari za kila mmoja kati ya Maalim Salman na Ahmed Iman Ali.
Viongozi hao wa kundi hilo la Somalia wanasakwa kwa kupanga mashambulio ya kigaidi likiwemo shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya mwezi Aprili.
Marekani imesema sita hao wamekuwa wakihusika katika kufadhili, kusajili wanachama na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa al-Shabaab.
Bw Ubaidah alifanywa kiongozi wa al-Shabaab mwaka jana baada ya mtangulizi wake Ahmed Godane kuuawa kwenye shambulio la ndege za Marekani.
Ubaidah amesisitiza kwamba kundi hilo bado ni tiifu kwa Al Qaeda, ingawa majuzi kuna kundi la wapiganaji hao lililojiunga na Islamic State

EU kutoa mabilioni kwa Afrika kupunguza wahamiaji



Wahamiaji wengi wamekuwa wakifa maji wakijaribu kufika Ulaya



Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanatarajiwa kutoa mabilioni ya euro kwa mataifa ya Afrika kuyawezesha kusaidia kupunguza mzozo wa wahamiaji Ulaya.

Tume ya Muungano wa Ulaya imesema itatoa €1.8bn (£1.3bn) na inatarajia mataifa zaidi ya EU yaahidi pesa zaidi.

Lengo la ufadhili huo ni kusaidia kusuluhisha matatizo ya kiuchumi na kiusalama ambayo huwafanya watu kutoroka mataifa ya Afrika. Aidha, zitatumiwa kuyashawishi mataifa ya Afrika kuwapokea watu ambao wamenyimwa hifadhi Ulaya.

Ahadi hiyo inatarajiwa kutolewa kwenye mkutano mkuu kuhusu wahamiaji unaofanyika Malta, na ambao ulipangwa baada ya meli iliyobeba wahamiaji kuzama Libya mwezi Aprili. Watu 800 walifariki

Watu 150,000 wamevuka bahari ya Mediterranean kutoka Afrika mwaka huu, wengi wakitua Italia na Malta.

Hata hivyo, mtazamo wa EU umebadilika tangu Aprili na kuangazia zaidi wakimbizi wanaotoka mashariki na hasa Syria, ambao wanawasili kwanza Ugiriki na kuvuka hadi Uturuki kisha kuelekea kaskazini kupitia bataifa ya Balkan.

Zaidi ya viongozi 60 kutoka Afrika na Ulaya, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, wanakutana Valletta, Malta kwa mkutano huo mkuu wa siku mbili kujadili uhamiaji.

Tume ya Muungano wa Ulaya itaweka pesa hizo €1.8bn kwenye "hazina maalum" kwa ajili ya Afrika na imehimiza mataifa wanachama kufikisha kiasi hicho cha pesa.

Hata hivyo, kuna shaka kuhusu iwapo mataifa hayo yatakubali wito huo

Tuesday, 10 November 2015

RAIS Jakaya Kikwete amewaonya baadhi ya viongozi wa serikali wastaafu wanaokwamisha utendaji wa serikali iliyopo madarakani kwa kutoa kauli vijiweni zinazoashiria kuwa imeshindwa kiutendaji huku wakisahau kuwa wanayoyasema hawakuyafanyia kazi kipindi cha uongozi wao.

Aidha ameonya tabia hiyo na kuwakumbusha viongozi hao kutambua kuwa kipindi chao cha kuwa madarakani kimekwisha na kazi kubwa walionayo ni kutoa ushauri kwa walioko madarakani badala ya kuwa vikwazo katika juhudi zao za kuleta maendeleo.

Rais aliyasema hayo leo, Ikulu, Dar es Salaam wakati akitoa hotuba mara baada ya kuzindua kitabu cha historia ya Rashid Mfaume Kawawa kiitwacho ‘Simba wa Vita katika Historia ya Tanzania, Rashid Mfaume Kawawa’ kilichoandikwa na Dk. John Magotti.

Magotti ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigambo, Dar es Salaam na amefanya kazi na Kawawa kwa muda mrefu.

Katika hafla hiyo iliyohusisha pia sherehe za kuzaliwa kwa Kawawa aliyetimiza miaka 83 leo na, viongozi wastaafu na walioko madarakani waliyohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Marais Wastaafu, Ali Hassan Mwingi na Benjamin Mkapa, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Jaji Joseph Warioba na John Malecela.

Wengine ni Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Bara), George Kahama, Mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere, Kingunge Ngombale Mwiru, viongozi wa taasisi za serikali na zisizo za serikali, Mashirika ya Kimataifa pamoja na familia ya Kawawa.

Kikwete akitoea mfano unyenyekevu wa Kawawa katika kipindi chote akiwa kiongozi katika ngazi mbalimbali nchini, alisema viongozi wengine wanakosa kufahamu kuwa kila jambo lina wakati wake hivyo wanajikuta wakitoa kauli za vijiweni zinazokwamisha maendeleo.

“Nakushuru Mzee Kawawa kwa kipindi chote cha kupanda na kushuka kwa uongozi wako hukuwa kama baadhi ya viongozi wengine wanaosahau wajibu wao wa kuwasaidia walioko madarakani na kujikuta wanapiga maneno vijiweni yasio mazuri,” alisema Kikwete na kuongeza;

“Inashangaza mtu huyo enzi za kuwa madarakani yeye hayo hakuyaona na wala kuyafanya…….., wewe siku zote umekuwa ukishauri pale unapoona mambo hayaendi sawa na tunakushuru sana Mzee wetu Kawawa.

Wapenzi wa jinsia moja watoroka Uganda


Mamia ya watu wa jamii ya jinsia moja nchini Uganda wamelitoroka taifa hilo ili kukwepa ubaguzi na mateso.
Lakini sasa wamekwama nchini Kenya ambapo hali sio shwari.
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza alisafiri hadi katika kambi moja ya wakimbizi ambapo vijikaratasi vilichapishwa katika kuta vikiwataka wakaazi kutojichanganya na watu wa jinsia hiyo.
Raia hao wa Uganda wamepiga kambi huko Kakuma kutoka taifa lenye amani.
Wakaazi wengine waliopo katika kambi hiyo wanatoka katika maeneo yaliyokumbwa na migogoro kama vile Sudan Kusini na Somalia
Mamia ya watu wa jamii ya jinsia moja nchini Uganda wamelitoroka taifa hilo ili kukwepa ubaguzi na mateso.
Lakini sasa wamekwama nchini Kenya ambapo hali sio shwari.
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza alisafiri hadi katika kambi moja ya wakimbizi ambapo vijikaratasi vilichapishwa katika kuta vikiwataka wakaazi kutojichanganya na watu wa jinsia hiyo.
Raia hao wa Uganda wamepiga kambi huko Kakuma kutoka taifa lenye amani.
Wakaazi wengine waliopo katika kambi hiyo wanatoka katika maeneo yaliyokumbwa na migogoro kama vile Sudan Kusini na Somalia

Vita vya jogoo vyasababisha vifo vya watu 10


Takriban watu 10 wamepigwa risasi na kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu jogoo yupi aliyeibuka mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico.

Miongoni mwa wale waliouawa ni ni mvulana mwenye umri wa miaka 12 aliyepigwa risasi katika mji wa Cuajinicuilapa.

Watu wengine 7 walijeruhiwa vibaya.

Uchunguzi wa awali uliashria kuwa mashabiki wa jogoo hizo mbili walitofautiana kuhusu ni yupi aliyeibuka mshindi.

Hata hivyo duru zinasema kuwa huenda ukumbi huo wa mapigano ya majimbi ulivamiwa na watu walikuwa wamejihami kwa bunduki.

Hadi kufikia sasa,haijulikani iwapo magenge yanayoshamiri mjini Guerrero ndiyo yaliyotekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Mwaka uliopita wanafunzi 43 walitoweka katika mji wa Iguala na kuweka tatizo la magenge katika majimbo ya Mexico katika rubaa za kimataifa

JIJI LA MBEYA LAAZA KUKUSANYA KODI

JIJI LA MBEYA LAJIPANGA KUKUSANYA KODI KATIKA MRADI WA SOKO JIPYA LA MWANJELWA




Kaimu Mkurugenzi jiji la Mbeya Dkt,Samuel Razalo.

 Na EmanuelMadafa, Mbeya
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imesema imejipanga vyema katika  kuhakikisha  mradi mkubwa wa soko jipya la mwanjelwa unasimamiwa kikamilifu kwa kufuata  taratibu za serikali sanjali na mikataba  iliyoingia na benki ya CRDB  kwa kipindi cha miaka 15.

Mradi  huo wa soko la kimataifa la Mwanjelwa lililopo jijini Mbeya  ujenzi wake imefikia  asilimia 99 hivyo upo katika hatua za mwisho za kukamilika kwake.

Akizungumza  ofisini kwake  , Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Razalo, amesema licha ya soko hilo kukamilika lakini mchakato wake wa uendeshaji utazingatia taratibu za halmashauri na mkataba walioingia na benki ya CRDB.

Amesema  hatua  hiyo, inatokana na halmashauri ya Jiji hilo kukopa kiasi cha shilingi Bilioni 13 kutoka benki ya CRDB na kufanikisha ujenzi wa soko hilo ambao umedumu kwa  zaidi ya miaka 10 tangu lilipoteketea kwa moto.


Amesema, benki hiyo kwa kukubaliana na halmashauri imepanga kiasi cha kodi kitakachopaswa kulipwa na wafanyabiashara  kuanzia shilingi elfu moja kwa siku hadi shilingi 500,000 kwa mwezi.

Amesema Wafanyabiashara ambao watatumia meza watatakiwa kulipa ushuru wa shilingi 1000 kwa siku huku wale wa maduka watalipa kiasi cha shilingi 500,000 kwa mwezi na wauza nyama watapaswa kulipa kiasi cha shilingi 400,000 kwa mwezi,”alisema.

Amesema , awali halmashauri hiyo ilipokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakiomba kupunguzwa kwa gharama za tozo hizo kwani ziko juu ukilinganisha na hali ya uhumi wa sasa.

Amesema, halmashauri iliyachukua maombi hayo na kuyawasilisha kwenye mamlaka husika ya benki ya CRDB hivyo wanasubili majibu na kuwataka wafanyabiasha kuwa wapole wakati wanasubili majibu hayo kutoka kwenye uongozi wa benki hiyo.

Soko la Mwanjelwa liliteketea kwa moto mwaka 2006 na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 2000 walionguliwa maduka yao na ujenzi wake kuanza mwaka 2008.

KAMPUNI YA SIMU YA TCCL YATOA VITABU KATKA SHULE ZA MISINGI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEA2T1Y9J-LjC9RBHrFnrzNdcM2wMsrDcQjmjfNSI8wiTE1qGRlrxhsfcubJvZJQe68axBjyLqxEsMBoTi6xse61EIFoso6QkM-TwAkqtSVQ3kfD-k4Csg8av4PqmqSvUx3Fb3Zh-Lyig/s1600/BL1.jpg

VYOMBO HABARI VIMECHANGIA KUFANYA UCHAGUZI KUWA WAZI NA HAKI NA HURU –NEC


Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.

MAKALA YA AMINA CHIFUPA NA HISTORIA YA KUSIKITISHA PAMOJA NA KIFO CHAKE


Marehemu mpiganaji Amina Chifupa.
  • Alifariki akiwa na umri wa miaka 26 tarehe 26 siku ya dunia kupiga vita dawa za kulevya
  • Alikuwa mwanaharakati wa kupinga biashara ya dawa za kulevya

Leo nimeona nijitokeze kuandika makala haya kupitia mtandao huu wa kijamii wa www.vitalisymalata.blogspot.com Makala ambayo ni Mbegu kwa waandishi wengine.
 
IKUMBUKWE kuwa Juni 26, 2007 ilikuwa ni siku ya Jumanne ambayo kwa watunza kumbukumbu za matukio yanayogusa jamii ni siku ambayo haitosahaulika kirahisi nchini Tanzania kufuatia Taaarifa za kushtua, baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Amina Chifupa Mpakanjia kufariki dunia.

Amina Chifupa alifariki akiwa na umri wa miaka 26 majira ya saa 3:00 katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) Lugalo Dar es Salaam kwa maradhi ya mfadhaiko wa akili yaani “depression”.

Majuma mawili kabla ya kifo chake Spika wa bunge la 9 Samuel Sitta aliwatangazia wabunge  kuhusu  kuugua kwa Amina na akawaomba wabunge wamwombee aweze kupona  haraka, hata mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi alipopata nafasi ya kuchangia hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu wa 2007/08 aliwasihi wabunge waendelee kumwombea Amina ili aweze kupona.

Kuugua kwa Amina kulianza kama mzaha huku kukigubikwa na habari za yeye kutalakiwa na mumewe Mpakanjia.

Ilidaiwa kwamba Mpakanjia alimtariki Amina baada ya kuwapo kwa habari kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA) hali iliyowafanya wachunguzi wa mambo  kuamini kuwa ndiko kulikomsababishia ugonjwa wa mfadhaiko wa akili.
Taarifa za madaktari wa Lugalo zilionyesha kuwa Amina alifariki kutokana na shinikizo la damu na kisukari, magonjwa ambayo haikuwahi kushuhudia wakati wa uhai wake.

Wengine wanadai kilichomuua Amina, mmoja ni kujitoa kwake mhanga  katika vita dhidi ya mihadarati  kwa maana ya dawa za kulevya.

Kwa ufupi ni mbunge ambaye alisimama kidete kutoboa siri za biashara za mihadarati na kuna wakati alipata kutishiwa na Polisi na kulazimika kumpa ulinzi  kwa muda kutokana na vitisho hivyo.
Amina alifariki akiwa na msuguano na baadhi ya viongozi wa UVCCM ambao walituhumiwa  kumwona kuwa tishio  katika nafasi ya uenyekiti wa Umoja huo ngazi ya Taifa.

Amina alizaliwa Mei 20, 1981 mjini Dar es Salaam, alisoma Shule ya Msingi Ushindi, Mikocheni Dar (1988-1994) kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Wasichana ya Kisutu, Dar (1995-1998). Elimu ya Juu ya Sekondari alisoma katika shule ya Makongo (1999-2001) kabla ya kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habri cha Royal (2001-2003) ambako alifuzu Diploma ya Uandishi wa Habari.

Mwaka 1999 alianza kazi ya Utangazaji wa Kituo cha Redio cha Clouds FM cha          Dar na aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mama Shughuli.

Katika CCM aliwahi kuwa Kamanda wa CCM wa umoja wa Vijana katika tawi la Mikocheni A jijini Dar na amekuwa Katibu wa Kamati ya Uchumi ya UVCCM mkoa wa Dar, aliwahi kuwa Mama Mlezi wa UVCCM na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) matawi ya Bunju na Mbagala.

MAZISHI YAKE
Maelfu ya wakazi wa Jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake siku ya Jumatano ya Juni 27, 2007 walifurika pembezoni mwa barabara za Bagamoyo na Kambarage wakiwa wameduwaa, wenye majonzi wakiupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM Amina Chifupa.

Mwili wake uliwasili nyumbani kwao Mkocheni saa 7:58 mchanaukiwa katika jeneza lililopambwa kitambaa kilichodariziwa na nakshi zenye rangi ya dhahabu ukitokea katika hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasili nyumbani hapo Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Shaban Simba aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika sala maalumu ya kumwombea marehemu na baadaye mwili huo ukaingizwa ndani ambako ulipokelewa kwa vilio vya nguvu kutoka kwa watu waliohudhuria.

Katika msiba huo siku hiyo wengi waliufananisha na msiba wa aliyekuwa mke wa watoto wa Malkia wa Uingereza, Marehemu Princess Diana au ule wa Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine.

Miongoni mwa waliohudhuria mwa waombolezaji waliojumuika  ni famila ya Chifupa, Mama Maria Nyerere, Mwanasiasa Mkongwe Mzee Rashid Kawawa (marehemu), Profesa Mark Mwandosya wakati huo akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Katibu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad, John Mnyika wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Vijana CHADEMA, baadhi ya wabunge, viongozi wa vyama vya siasa na wananchi wa kawaida.

Nyumbani kwa mzee Khamis Chifupa, baba mzazi wa Amina watu walikuwa wamefurika licha ya ukubwa wa eneo la makazi hayo na hivyo kusababisha msongano.

Hali hiyo ilisababisha Meya Manispaa ya Kinondoni  wakati huo Salum Londa kuingilia kati  na kusaidia  kamati ya mazishi  kuwapanga na kuwatuliza waombolezaji.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam wakati huo Hemed Mkali alisema kuwa kifo cha Amina kimedhihirisha kuwa kweli alikuwa anaumizwa  na matatizo ya dawa za kulevya nchini kwani kimetokea siku iliyotengwa na dunia kupiga vita dawa za kulevya.

Meya wa Jiji la Dar wakati huo Adama Kimbisa alisema Amina alikuwa kijana mwenye kusimamia  ukweli, haki na maadili. Kimbisa alisema katika vikao  mbalimbali jambo na kulitetea kwa kufuata  misingi ya haki.

Mkurugenzi wa Clouds FM Joseph Kusaga alimwelezea Amina Chifupa ilikuwa ni hazina kwa taifa hasa kwa wasichana wadogo kutokana na kipaji alichojaliwa kujiamini katika maisha yake tangu utotoni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati huo Profesa Mark Mwandosya alisema kifo cha Amina kimeacha changamoto kubwa kwa serikali na wadau wengine kushughulikia tatizo la kushamiri kwa dawa kulevya nchini.

Kwa upande wake Maalim Seif Shariff Hamad Katibu Mkuu wa CUF alisema Amina alishughulikia kero mbalimbali zinazoiathiri jamii bila kujali itikadi za kisiasa, alikuwa mwanasiasa chipukizi aliyejitolea kushughulikia kero za wananchi bila woga.

Tutamkumbuka kwa ucheshi na uwezo mkubwa wa kujenga hoja mbalimbali ndani na nje ya Bunge. Katika kipindi kifupi akiwa Mwanasiasa kijana, aliweza kusimama na kujipembua na wabunge wengine kwa kusimama kidete kupiga vita biashara ya mihadarati ambayo alaiamini inaua vijana ambao ni viongozi wa kesho.   

Alipata Ubunge Desemba 28, 2005 akitakiwa kudumu katika bunge kwa miaka mitano hadi Desemba 27, 2010. Namba yake ya Usajili kama Mbunge ilikuwa ni 1313.

Alizikwa majira ya saa 10 jioni ya Juni 28, 2007 kijijini Lupembe Wilayani Njombe mkoa wa Iringa wakati huo, karibu kabisa na eneo alilokuwa akiishi bibi yake.

Spika wa Bunge la 9 Samuel Sitta aliongoza mazishi hayo ayaliyohudhuria na watu wa kada mbalimbali na watu mashuhuri.

Suu Kyi asema uchaguzi ulikuwa wa haki

Kiongozi wa upinzani Myanmar Aung San Suu Kyi ameambia BBC kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki.
Kwenye mahojiano ya kipekee, Bi Suu Kyi aliwapongeza watu wa Myanmar. Matokeo ya mapema yanaonyesha chama chake cha National League for Democracy (NLD) kitapata ushindi mkubwa.
Chini ya katiba ya chini hiyo hawezi akawa rais, lakini amesema kwamba kama kiongozi wa chama atamteua rais.
Uchaguz huo umechukuliwa na wengi kuwa ulio wa kidemokrasia zaidi katika miaka 25, baada ya miongo kadha ya uongozi wa kijeshi.
Matokeo rasmi ya uchaguzi yalianza kutolewa Jumatatu, lakini matokeo kamili yanatarajiwa kuchukua siku kadha.
Chama cha NLD kimeshinda viti vingi vya ubunge kati ya vile ambavyo matokeo yake yametangazwa.
Chama tawala cha Union Solidarity Development Party (USDP) kinachoungwa mkono na jeshi, kimekuwa madarakani tangu 2011 taifa hilo lilipoanza shughuli ya mpito kutoka utawala wa kijeshi hadi uongozi wa kiraia.
Alipoulizwa iwapo uchaguzi huo huenda ukahujumiwa, Bi Suu Kyi alijibu kwamba watakaofanya hivyo watakuwa wanahujumu mapenzi ya raia

Zanzibar kunii malizeni tofauti zenu

Zanzibar:Shein akutana na Maalim Seif

Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano

uliowaleta pamoja rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad ukifanyika.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mkutano huo wa faragha katika ikulu ya rais ulihudhuriwa na marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid karume.
Ni mara ya kwanza kwa Dkt Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni makamu wa rais wa kisiwa hicho kukutana tangu tume ya uchaguzi.
Kushirikishwa kwa marais hao wa zamani ni thibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa zinazoendelea katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua mgogoro wa kikatiba.
Wanachama wa jumuiya ya kimataifa pia wanadaiwa kushiriki katika kumaliza tatizo hilo.
Hakuna habari zilizotolewa kutoka pande zote mbili lakini duru za serikali zimethibitisha kwamba mazungumzo hayo yalifanyika kwa faragha.
Makamu wa rais wa pili Seif Ali Idd pia amedaiwa kuhudhuria mkutano huo kulingana na duru hizo.
Bw Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kifupi kabla ya kuteuliwa kuwania urais mwaka 1985 huku Karume akiliongoza eneo hilo kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2010.
Maafisa wa ikulu ya rais visiwani Zanzibar hawakuwa tayari kuzungumzia kuhusu yalioafikiwa katika mkutano huo.
Wale kutoka CUF hata hivyo wamesema kuwa majadiliano yalikuwa mazuri kwa maslahi ya raia wa muungano wa Tanzania.

Monday, 9 November 2015

Ufaransa yaeleza wasiwasi kuhusu hali Burundi

Ufaransa imependekeza hatua zichukuliwe kusitisha mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Burundi.
Taifa hilo liliwasilisha mswada wa mapendekezo kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu likieleza wasiwasi wake kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.
Machafuko hayo ndiyo mabaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka kumi.
Ghasia zilianza Aprili baada ya maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza angewania urais kwa muhula wa tatu. Jumamosi, watu tisa waliuawa kwa kupigwa risasi katika baa moja mji mkuu wa Bujumbura.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alishutumu mauaji hayo ya Jumatatu na kusema mmoja wa waliouawa alikuwa afisa wa UN.
Afisa mmoja wa polisi anadaiwa kujeruhiwa na takriban watu wawili kuuawa huku polisi wakindelea kusaka silaha katika nyumba za wakazi mitaa ambayo ni ngome ya wapinzani.
Rais wa Rwanda Paul Kagame amekosoa viongozi wa Burundi kutokana na wanavyoshughulikia mzozo nchini humo na kuna wasiwasi huenda kukatokea mauaji ya kimbari, mwandishi wa BBC Alastair Leithead anasema.
Naibu balozi wa Ufaransa katika UN Alexis Lamek aliambia AFP kwamba Ufaransa “imehofishwa sana na yanayoendelea Burundi kwa sasa.”
Ujumbe wa Ufaransa katika UN ulisema mashauriano kuhusu azimio lake yangeanza Jumatatu jioni.
Shirika la International Crisis Group lenye makao yake Brussels limeonya kuwa lugha inayotumiwa kwa sasa Burundi “inashabihiana sana” na iliyotumiwa Rwanda kabla ya mauaji ya halaiki ya 1994.
Machafuko yalianza Aprili Nkurunziza aliposema muhula wake wa kwanza wa urais haukufaa kuhesabiwa katika kutekeleza takwa la kikatiba la rais kuhudumu mihula miwili pekee kwa kuwa alichaguliwa na wabunge wakati huo.

Rais wa Nigeria afukuza kazi mwingine.

Zifahamu tabia sita za wachezaji wa Kibrazil ambazo karibia wote huwa wanazo …


Jose Mourinho retains Chelsea owner Abramovich's support

Chelsea manager Jose Mourinho still retains the support of Blues owner Roman Abramovich and his position is not under immediate threat

Kagame awashutumu viongozi wa Burundi


Rais wa Rwanda Paul Kagame ameshutumu vikali viongozi wa Burundi kutokana na mauaji yanayoendelea nchini humo nakuonya kuwa huenda kukatokea mauaji ya halaiki
Bw Kagame ameshangaa ni vipi viongozi wa taifa hilo jirani "wanaweza kuruhusu wananchi wao kuuwawa kiholela".
Rais Kagame alisema hayo Ijumaa, lakini matamshi yake hayakutangazwa hadi mwishoni mwa wiki, akionekana sana kumlenga Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Akizungumza kwa Kinyarwanda Rais Kagame alisema: ''Tazama nchi jirani kama Burundi, maisha yao yamesimama kabisa. Lakini sababu ni ipi? Wana historia inayofanana na yetu.
Ila viongozi wao wapo kwa ajili ya kuua wananchi kuanzia asubuhi hadi jioni."
''Rais akajifungia sehemu isiyojulikana, hakuna anayejua sehemu alikojificha, hakuna anayezungumza naye, huyo anaongoza watu vipi?" alisema Bw Kagame, akihutubu katika hafla ya kuwatunuku Wanyarwanda waliosaidia kuwaficha na kuwaokoa Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari 1994 pamoja na wanaharakati wanaotetea umoja na maridhiano miongoni mwa Wanyarwanda.
''Watu wanakufa kila siku, maiti zinabururwa barabarani. La kusikitisha ni kuwa bara la Afrika lina ugonjwa wake lenyewe kiasi kwamba hata nitalaumiwa eti nimekosea kuitaja nchi nyingine, eti ningecheza diplomasia au siasa. Siyo haki mimi nitasema wazi. Viongozi wanashinda wakiua watu, maiti zinatapakaa sehemu zote; wakimbizi wanarandaranda sehemu zote watoto, wanawake ....kisha unasema ni siasa. Hiyo ni siasa gani?"
Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi umedorora sana tangu Bw Nkurunziza atangaze kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu, hatua iliyopingwa na wapinzani.


Mwezi uliopita, Burundi ilimfurusha mwanabalozi mmoja kutoka Rwanda ikimtuhumu kwa kuhujumu usalama wa nchi hiyo.
"Utasema kuwa ni nani aliyesababisha matatizo ya Burundi? hata kukiwa na mtu anayekutakia mabaya atavutiwa na ubaya wako unaotenda...Hata kama ni mtu kutoka Rwanda anayesababisha machafuko nchini Burundi, bila shaka atavutiwa na maovu ya viongozi wa Burundi wanayotendea wananchi wao. Shida ni ya Warundi wenyewe," alisema Bw Kagame.
"Tatizo ni kwamba hawakupata somo kutoka kwetu (Rwanda), kutokana na yaliyosibu taifa letu wangepata somo hasa kutokana na baadhi ya Warundi wenyewe kuhusika katika yale yaliyolisibu taifa letu.
Afrika sijui tunaugua ugonjwa upi?"
Hayo yamejiri siku moja baaya watu 9 kuawa usiku na watu wenye silaha, ndani ya baa moja katika mji mkuu wa Bujumbura.
Askari wa usalama wanafanya msako katika kila nyumba, kwenye mitaa inayoonekana kuwa ni ngome za upinzani, baada ya muda uliowekwa na serikali kwa watu kusalimisha silaha zao kumalizika.
Watu takriban 20 wameuwawa nchini Burundi katika juma lilopita, huku maelfu ya watu wakitoroka makwao

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YAFANA SANA JIJINI MONTREAL, CANADA

 RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, ATEUA UONGOZI MPYA WA MUDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

“ Rais  amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko”.  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kwenye wodi ya sewahaji, kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam leo wakati wa ziara yake ya kushtukiza .

UJASIRI WA WANASHERIA WASAIDIA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI WA JINSIA SOKO LA TABATA MUSLIM JIJINI DAR ES SALAAM

 Katibu wa soko la Tabata Muslim lililopo Manispaa ya Ilala, John Nombo (kushoto),  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA ASHIRIKI HAFLA YA DUA YA KUOMBEA TAIFA AMANI, JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa hafla maalumu ya kuliombea Taifa Amani, iliyoandaliwa na Kamati ya Amani,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.