Wednesday, 22 June 2016

HAKUNA MAJERUHI YANGA -MURO.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENCHI la Ufundi la Kikosi cha Yanga limeweka wazi kuwa hali ya beki wake wa kushoto Oscar Joshua aliyeumia katika mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia anaendelea vizuri na atarejea uwanjani tena Jumanne kukipiga na TP Mazembe huku beki wa kulia Juma Abdul anaendelea vizuri na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mepesi.

Abdul alikosa mechi ya awali baada ya kuwa majeruhi kwa kuumia sehemu ya kifundo cha mguu na kuukosa mchezo wa kwanza na nafasi yake ikichukuliwa na Mbuyi Twite. Hata hivyo kwa sasa anaendelea vizuri na daktari ameweka wazi kuwa anaweza kuanza mazoezi na timu itakaporejea ataungana na wenzake.

Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro (Pichani)amesema kuwa Joshua anaendelwa vizuri na watakaoukosa mchezo huo ni Beki wa kushoto Mwinyi Haji aliyepata kadi nyekundu pamoja na mshambuliaji Amisi Tambwe mwenye kadi mbili za njano alizozipata kwenye mchezo wa marudiano na Segrada Esperanca ya Angola na wa hatua ya makundi na Mo Bejaia.

"Ni wachezaji wawili tu ndiyo watakaokosa mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao ni Mwinyi anayetumikia kadi nyekundu na Tambwe mwenye kadi mbili za njano, kwahiyo katika mchezo huo Oscar atarejea tena uwanjani na Abdul anaendelea vizuri ameanza mazoezi mepesi mepesi na pindi timu itakaporejea ataungana nao,"amesema Muro.

Kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi katika jiji la Antalya nchini Uturuki ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao utapigigwa Siku ya Jumanne Juni 28 na unatarajiwa kuwa wa ushindani wa hali ya juu hasa baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa awali na wakihitaji matokeo na TP Mazembe wakitaka ushindi ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali.

WAZIRI WA AFYA , MAENDELEO YA JAMII , JINSIA, WAZEE NA WATOTO ATEMBELEA VIJIJI VILIVYOKUMBWA NA MLIPUKO WA UGONJWA USIOJULIKANA WILAYANI KONDOA.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe, Wilayani Kondoa.

Katika ziara hilyo ameambatana na wataalam mbalimbali ambao wameweka kambi kwenye vijiji hivyo ili kufuatilia wagonjwa majumbani.vile vile ametembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya kondoa.
Mbunge wa Kondoa,Juma Nkamia akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kondoa Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kutembelea vijiji vilivyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa usiojulikana katika kijiji cha mwaisabe,Wilayani Kondoa

Jeshi la Ujerumani lapanuwa operesheni yake Mediterenia

Jeshi la Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Bundeswehr, litakuwa siku za mbele linalinda sio tu mwambao wa Libya, bali pia kuwaandama wafanyabiashara haramu wa silaha. Baraza la mawaziri limekubaliana operesheni ya ukaguzi wa manuari za Umoja wa Ulaya katika Bahari ya Mediterenia, inayojulikana kwa jina la Sophia, ipanuliwe. Juhudi za kusimamia utekelezaji wa vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa zimelengwa kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali wa Dola la Kiislam wasipatiwe silaha katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini. Zaidi ya hayo, kwa kupanuliwa shughuli za ukaguzi za manuari za Umoja wa Ulaya, itapatikana njia pia ya kupatiwa mafunzo walinzi wa fukwe za Libya. Uamuzi wa baraza la mawaziri unabidi uidhinishwe na bunge la shirikisho, Bundestag. Hata hivyo, serikali kuu ya muungano inadhibiti wingi wa viti bungeni.

Hatima ya Umoja wa Ulaya inafungamanishwa na matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza



Rais Francois Hollande wa Ufaransa anasema mustakbali wa Ulaya unategemea matokeo ya kura ya maoni ya Uingereza kama itasalia au itatoka katika Umoja wa ulaya. Rais Hollande amesema hayo baada ya mazungumzo pamoja na waziri mkuu wa Slovakia Robert Fico, mnamo mkesha wa kura ya maoni ambapo Waingereza watachagua kama wanataka nchi yao itoke au Brexit au isalie katika Umoja wa ulaya. Rais Hollande anasema Paris itauangalia uamuzi wa waingereza kuwa "usiobadilishika" na kuongeza "London itakumbwa na hatari kubwa ikiwa haitokuwa na njia ya kuingia katika soko la pamoja. Rais Francois Hollande wa Ufaransa alikuwa kila mara akiitetea umuhimu wa Uingereza kusalia katika Umoja wa Ulaya. Wito kama huo umetolewa pia na kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo. "Bila ya shaka ninataka Uingereza iendelee kuwa mwanachama wa Umoja wa ulaya lakini uamuzi wanao wananchi wa Uingereza" amesema Kansela Merkel mbele ya maripota baada ya mazungumzo pamoja na Waziri Mkuu wa Poland, Beata Szydlo

Putin ailaumu NATO kwa "uchokozi"

Rais Vladimir Putin wa Urusi ameilaumu Jumuiya ya Kujihami ya NATO kwa kile alichokiita "matamshi makali" na "harakati zake za uchokozi" karibu na mpaka wa Urusi. Rais Putin ameonya visa kama hivyo vitailazimisha Moscow kuimarisha nguvu zake za kijeshi. "NATO inazidisha maneno na harakati za uchokozi karibu na mipaka yetu," amesema Rais Putin mbele ya wabunge wa nchi hiyo waliokusanyika katika kumbukumbu za miaka 75 tangu Ujerumani ya zamani ya Wanazi ilipoivamia Usovieti. Rais Putin amezikosoa nchi za Magharibi kwa kukataa mchango wa Urusi kusaidia kukabiliana na adui wa pamoja ambae ni ugaidi wa kimataifa, kama walivyolipuuza onyo la Soviet Union kuhusu Hitler na kama wanavyojaribu kuitenga Moscow katika mzozo wa Ukraine. Uhusiano kati ya Urusi na nchi za Magharibi umepooza na kufikia kiwango cha vita baridi tangu Moscow ilipolikalia eneo la Crimea mwaka 2014 na kuunga mkono vuguvugu la wanaotaka kujitenga mashariki ya Ukraine.

Ibrahimovic kustaafu soka ya kimataifa


Nyota wa Sweden Zlatan Ibrahimovich ametangaza kwamba atastaafu katika soka ya kimataifa baada ya michuano ya Euro 2016.
Taifa lake linakutana na Ubelgiji katika mechi ya mwisho ya kundi E siku ya jumatanoambayo huenda ikawa mechi yake ya mwisho kwa taifa lake.
Alisema:Ninajivunia kile nilichofanikiwa kupata na kila mara nitatembea na bendera ya Sweden.
Klabu ya Manchester United imehusishwa pakubwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ambaye alikuwa ajenti huru baada ya kuondoka klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa .

Wachezaji wa Albania kuzawadiwa paspoti za kidiplomasia


Taifa la Albania limesema kuwa litawazawadi wachezaji wake wa soka pasipoti za kidiplomasia kwa kuishinda Romania 1-0 katika michuano ya Euro2016.
Taifa hilo halijashiriki katika mchuano wowote wa soka wenye tajriba ya hali ya juu.
Lakini haijulikani iwapo taifa hilo litafuzu kwa raundi ya pili nchini Ufaransa.
Timu hiyo itapewa zawadi zaidi ya Euro milioni moja pamoja na pasipoti hizo mpya,serikali imesema.
Albania ilipoteza mechi zake mbili na kuwa wa tatu katika kundi lake.
Waziri mkuu wa Albania Edi Rama alishuhudia furaha iliokuwepo nchini humo baada ya Armando Sadiku kufunga bao la kichwa na la ushindi dhidi ya Romania katika kipindi cha kwanza cha mechi.

CCM YAWASILISHA KWA MSAJILI WA VYAMA MATUMIZI YA UCHAGUZI MKUU

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo akimkabidhi vielelezo vya CCM vya matumizi ya Uchaguzi mkuu uliopita, kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala  Galasia Simbachawene, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na habari na Bashir Nkoromo)

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana,  na kuwa chama cha pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.

Ujumbe wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa Masijala  Galasia Simbachawene.
Akikabidhi hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25, 2016.
"Sisi hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee kuwa chama cha kuigwa ", alisema Mamilo.
Mamililo aliwasilisha hati na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.
Alisema, uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.
Kulingana na Sheria ya Uchaguzi, chama kinatakiwa kisitumie ghara inayozidi sh. bilioni 17, na kikilazimika kuzidi kiwango hicho kisididi zaidi ya asilimia 15 ya kiwango kinachotakiwa, huku kwa upande wa wagombea kiasi kinachotakiwa ni sh. bilioni  saba na kwa wabunge sh. milioni 33 hadi 88 kulingana na mazingira ya jimbo.

KAMISHNA MSTAAFU SULEIMAN KOVA AAGWA RASMI KIJESHI BAADA YA KUSTAAFU


 Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi
 
 Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi
 
 Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa  sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki.
 
 Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiwa ni ishara ya kumuaga zilizofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi nakuongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki
 
Gwaride Maalumu la Kumuaga Kamishna Mstaafu Suleiman Kova likipita mbele yake kwa mwendo wa haraka wakati wa Sherehe za kumuaga rasmi baada ya kustaafu utumishi.Sherehe hizo zilifanyika katika chuo cha Polisi Moshi (Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

Ethiopia yatupa mipira ya kondomu milioni 69


Ethiopia inatarajiwa kutupa mipira ya kondomu milioni 69, iliyonunuliwa kwa kima cha dola milioni mbili kutoka na ubora wa chini wa mipira hiyo.
Hii ilitangazwa na mfuko wa serikali unaohusika na madawa nchini humo.
Hatua sasa zinachukuliwa kuhakisha kuwa fedha zilizotumika na zilizotolewa na shirika moja la kimataifa linalofadhiliwa na Umoja wa Mataifa
zimerejeshwa

Korea Kaskazini yalipua tena makombora


Korea Kusini inasema kuwa majirani zao Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena, wameifanyia majaribio makombora yake mawili, hatua ya wazi ya kuonesha kukiuka hatua Umoja wa mataifa kuiwekea taifa hilo vikwazo vya kiuchumi. Taarifa zasema kombora la kwanza halikufanikiwa huku la pili likisafiri umbali wa kilomita mia nne.
Msemaji wa Waziri wa Umoja wa taifa wa Korea Kusini Joeng Joon-hee amesema majaribio hayo ni kukiuka vikwazo.
"Ulipuaji huo makombora kwa kutumia Teknolojia ya angani unakiuka maazimio ya Umoja wa mataifa. NIa ni uchokozi dhidi yetu. Tunashauri ni vyema kwa Korea Kaskazini kuzidisha nguvu katika kuimarisha amani katika eneo la rasi ya Korea na kwa maisha ya watu wake ambayo Korea kaskazini imekuwa ikisititiza kila wakati." Amesema
Naye waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amelaani hatua hiyo Korea ya Kaskazini.
"Leo kumelipuliwa makombora kwa kutumia teknolojia ya angani iliyotumika zamani huu ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa. hatutarusu na tutaandaa azimio la kupinga hatua hiyo," amesema Waziri Mkuu huyo

2 people killed in violent South Africa



   


The two men reportedly shot and 40 were injured during the demonstrations of clashes in the South African capital Pretoria.

The protest is a protest action in the country's ruling party, the African National Congress (ANC) to appoint a candidate for mayor in August.

Looting at stores including those owned by immigrants, has continued throughout the day despite having a low level compared to yesterday and Monday

Moise Katumbi ahukumiwa miaka 3 jela

Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi.
Pia alipigwa faini ya dola milioni 6.
Katumbi hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.
Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali.
Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba

Tuesday, 14 June 2016

Babake Reeva amtaka Pistorius kulipia alichotenda

Baba wa mwanamitindo wa Afrika Kusini ambaye aliuawa Reeva Steenkamp, amezungumza mahakamani kwa mara ya kwanza akisema kuwa muuaji wa Reva, Oscar Pistorius lazima alipie yale aliyoyatenda.
Akizungumza mahakamani huku amejawa na majonzi, bwana Steenkamp alisema kuwa familia yake imetaabika kutokana na kuuawa kwa Reeva.
Alisema anaamini kuwa bintiye alikuwa amegombana na Oscar Pistorius usiku ambao aliuawa miaka mitatu iliyopita.
Image copyright Reuters
Image caption Reeva Steenkamp na Oscar Pistorius
Bwana Steenkamp wakati huo hakuwa na afya nzuri kuweza kuhudhuria kesi.
Mahakama mjini Pretoria itaamua hukumu ambayo itampa Oscar baada ya hukumu ya kwanza kubadilishwa na kuwa mauaji.

Profesa Muhongo aelezea mikakati Sekta za Nishati na Madini, Benki ya Dunia yafurahishwa na utekelezaji wake

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongoza kikao kilichoshirikisha Watendaji kutoka Benki ya Dunia pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA).
Mtendaji Kutoka Benki ya Dunia anayeshughulikia mazingira Vladislav Vucetic, akielezea mikakati ya benki hiyo katika ushirikiano wake na Serikali ili kupanua sekta za nishati na madini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto waliokaa mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto waliokaa mbele) wakifuatilia kwa makini maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo( hayupo pichani) katika kikao hicho.


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameelezea mikakati ya Serikali katika uboreshaji wa sekta za nishati na madini na kuongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) katika uboreshaji wa sekta hizo ili ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokutana na Watendaji kutoka Benki ya Dunia pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA)

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI ZA JUU MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ESALAAM

Gwaride la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la uvishaji cheo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani)

Mkapa awataka watanzania kufanya kazi kwa bidii.

Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa akikata utepe kuzindua kitabu cha kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam kushoto ni Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala. 
Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama cha ACT wazalendo Bi. Anna Mghwira akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.Picha na Ally Daud-Maelezo

Na Ally Daud- Maelezo

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Huyo Mstaafu ameyasema hayo katika mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali baada ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali " alisema Dkt Mkapa.

Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwal. J.k nyerere. Mbali na mkutano huo pia kulikua na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini.

Mkutano huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umeudhuriwa na wawakilishi Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndan na nje ya nchi.

Kwa upande wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala alisema kuwa mkutano huo unalenga kudumisha na kuendeleza aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k Nyerere.Mbali na hayo amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha Mwalimu.

DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA RASMI KESHO


DIRISHA la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) na ligi Daraja la kwanza (FDL) litafunguliwa rasmi kesho huku timu zikishauriwa kufanya usajili kwa umakini mkubwa na linatarajiwa kufungwa Agosti 6 ambapo usajili huo utaenda sambamba na semina elekezi kwa viongozi wawili wa timu zinazo shiriki ligi kuu, ligi daraja la kwanza pamoja na ligi daraja la pili na  wanaotakiwa kuhudhuria semina hiyo ni Katibu mkuu wa klabu pamoja na Afisa usajili.

 Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa semina hiyo itahusu matumizi ya mifumo ya usajili kwa njia ya mtandao (TMS) kwani msimu ujao ni lazima kila timu iwasilishe usajili wa wachezaji wake kwa mfumo wa TMS kama FIFA walivyoelekeza.

"Misimu miwili iyopita tulianza kuutumia mfumo huu lakini haujaonesha kufanikiwa sana na ndio maana imeitishwa semina hii kwani kwa msimu ujao wachezaji watakaotambuliwa ni wale watakaosajiliwa kwa mfumo wa TMS", amesema Alfred. Semina hiyo itaanza siku ya jumatatu semina itakayowahusu viongozi wa ligi kuu, Jumanne itakuwa kwa ajili wa viongozi wa Ligi daraja la kwanza huku ikimalizika kwa viongozi wa ligi daraja la pili siku ya Jumatano.

Kuanzia leo hadi Juni 30 kutahusisha uhamisho wa wachezaji huku timu hizo pia zikitakiwa kuweka wazi wachezaji wanaowaacha  ili waweze kusajiliwa na timu nyingine endapo wanawahitaji. Kipindi cha Agosti 7 hadi 14 kitatumika kwa ajili ya mapingamizi kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, huku hatua ya pili ikianza Agosti 17 hadi Septemba 7. 

Na pingamizi la hatua ya pili zitaanza  Septemba 8 hadi Septemba 14 na Septemba 15 hadi 17 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili.

TFF pia imezitaka klabu zinazoshiriki ligi kuu (VPL), ligi daraja la kwanza (FDL) pamoja na daraja la pili (SDL) kutaja viwanja vyake vya nyumbani kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Timu hizo zinatakiwa kuwasilisha taarifa ya viwanja watakavyovichagua kabla ya Juni 20 mwaka huu.

Klabu hizo zinatakiwa kupeleka vipimo vya viwanja husika ili TFF kupitia kamati ya mashindano ijiridhishe kama vitafaa kutumika kwa ajili ya ligi husika na timu zinazoshiriki mashindano hayo pia zinatakiwa kuambatanisha vipimo hivyo na aina ya nyasi, idadi ya vyumba, uwezo wa mashabiki wanaoweza kuingia pamoja na jina la mmiliki.

"TFF itahitaji kupata taarifa mapema na iweze kufanyia kazi kwani ni muhimu kukagua viwanja hivyo kama vina sifa zinazostahiki na hata kama ikitokea mechi zimepangwa usiku basi timu ziweze kucheza", amesema Alfred.


Tumezielekeza kwamba iwapo timu haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa wa jirani. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (3) Ligi Kuu Tanzania Bara toleo la 2016/17.

MAHAKAMA YA KISUTU YATENGUA UDIWANI WA CHADEMA KATA YA SARANGA





Na Mwene Said, Globu ya Jamii, Dar es Salaam.




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetengua matokeo ya kiti cha diwani wa Kata ya Saranga, Efraim Kinyafu (CHADEMA), baada ya kubaini kwamba uchaguzi ulikiuka taratibu katika kuhesabu kura.




Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Mdoe dhidi ya diwani huyo Kinyafu na msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).




Hukumu hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema ambaye kwa sasa amehamishiwa kituo kingine cha kazi na ilisomwa kwa niaba yake na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.




“Mahakama baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili, imebaini kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika kuhesabu kura inatengua matokeo ya uchaguzi wa kata ya Saranga” alisema Hakimu Mashauri.




Mdoe alifungua kesi hiyo akidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kuhesabu kura akilalamikia kituo kimoja na kuiomba mahakama kuamua vyovyote itakavyoona inafaa na itamke uchaguzi haukuwa wa huru na wa haki.




Akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Fredrick Kihwelu, alidai mteja wake hajaridhika na hukumu hiyo hivyo watakata rufani kuipinga.




Alidai wataomba mahakamani wapatiwe mwenendo wa kesi ili waweze kuwasilisha sababu za kukata rufani.




Wakili huyo alidai mdai huyo alikuwa halalamikii kushindwa kwa kuwa wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, alikiri kushindwa kwa tofauti ya kura zaidi ya 500.




Alidai katika kituo ambacho alikuwa akilalamikia mdai huyo kulikuwa na wapigakura 68, hivyo hata kama kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kuhesabu kura kusingeweza kubadili matokeo yote.



Wakili huyo alishauri kwamba aliyepaswa kusahihishwa kwa kukiuka taratibu ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kesho na keshokutwa iwe makini kwa kutorudia makosa na sio mdaiwa wa kwanza (Kinyafu)

Mapigano yaikumba Eritrea na Ethiopia



Eritrea na Ethiopia zimetupiana lawama kwa kuanzisha mapigano mwishoni mwa juma baina ya majeshi yake katika eneo la mpakani linalotumiwa na nchi zote mbili la Tsorona.
Eritrea na Ethiopia zimetupiana lawama kwa kuanzisha mapigano mwishoni mwa juma baina ya majeshi yake katika eneo la mpakani linalotumiwa na nchi zote mbili la Tsorona, ikiashiria kuendelea kwa mgogoro wa mpaka uliochochea vita baina ya mataifa hayo mawili mwaka 1998 hadi 2000.
Ethiopia imesema kwamba hali ilitulia hapo jana, baada ya wakaazi wanaoishi upande wa nchi hiyo kutoa taarifa za kusikika kwa milipuko iliyodumu siku nzima ya Jumapili hadi Jumatatu asubuhi.
Eritrea nchi iliyo Pembe ya Afrika, ilijipatia uhuru kutoka mikononi mwa Ethiopia mnamo mwaka 1991. Takribani watu 70,000 waliuawa katika vita ya kugombea mpaka baina ya mataifa hayo mawili.
Waziri wa habari wa Eritrea amesema kwamba serikali ya Ethiopia ilianzisha mashambulizi dhidi ya nchi yake katika eneo la mbele la Tsorona.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa katibu mkuu Ban Ki-moon anao wasiwasi juu ya mapigano hayo na tayari anataka kuzifikia pande zote mbili.
Amesema kwamba "katibu mkuu anazitaka serikali zote kujizuia na kufanyia kazi utatuzi wa tofauti zao kwa njia ya amani, ikiwemo utekelezaji wa makubaliano ya amani waliyosaini mwaka 2000" amesema waziri huyo.
Rais wa Eritrea Isayas Afewerki Rais wa Eritrea Isayas Afewerki
Umoja wa Mataifa ulipeleka kikosi cha kufuatilia makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano mwaka 2000 katika mpaka baina ya nchi hizo mbili , lakini hata hivyo ilikiondoa kikosi hicho 2008 kutokana na vikwazo vilivyowekwa na Eritrea na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ujumbe huo.
Ethiopia kwa upande wake nayo imekanusha kuanzisha chokochoko ikisema kwamba ni majeshi ya Eritrea yaliyoanzisha fujo hizo.
Waziri wa habari wa Eritrea Yemene Ghebremeskel hakuwa na maoni juu ya majeruhi au taarifa nyingine juu ya mashambulizi hayo.Maafisa wa Ethiopia nao hawajatoa taarifa ikiwa kulikuwa na majeruhi.
Umoja wa Mataifa unaishutumu Eritrea kwa ukiukwaji wa muda mrefu wa haki za huduma za kitaifa ambapo raia wa nchi hiyo hutumia muda mrefu wakilipwa ujira mdogo kwa mujibu wa sheria.
Charlotte King, mchambuzi mwandamizi wa Afrika katika kitengo cha intelijensia ya uchumi anasema wakosoaji wa Eritrea wataona kama nchi hiyo inajaribu kukwepa tahadhari ya jumuiya za kimataifa dhidi ya uhalifu wa ubinaadamu na kuhalalisha mahitaji yake ya kijeshi.
Eritrea iliyo na vikwazo vya Umoja wa mataifa inasema mataigfa yenye nguvu yameshindwa kuishinkiza Ethiopia kukubaliana na usuluhishi wa kimataifa unaotawala mpaka huo. Ethiopia imesema inataka mazungumzo kwa ajili ya utekelezaji.

Muuaji wa Orlando alitembelea kilabu ya wapenzi wa jinsia moja




Ripoti kutoka Orlando Marekani zasema Omar Mateen, mtu aliyewafyatulia risasi na kuwaua watu 49 katika klabu moja ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, alikuwa akitembelea klabu hiyo iitwayo Pulse mara kwa mara.
Wahudumu na meneja wa klabu hiyo amenukuliwa na magazeti ya Marekani akisema kuwa, ameshawahi kumuona Mateen, hata akinywa pombe katika eneo hilo.
Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za ugomvi wa mara kwa mara na kutaka kupigana na watu na wala hakuwa na itikadi kali za kidini.
Mke huyo pia anaongeza kusema kuwa, wakati mwengine alionekana kutokuwa na akili timamu.
Baadhi ya wateja wa klabu hiyo wanasema kwamba, alikuwa katika mtandao wa watu wa wapenzi wa jinsia moja.
Waandishi wa habari nao wanasema kuwa, taarifa zinazofichua alivyokuwa Mateen, zinaibua maswali chungu nzima kuhusiana na kiini cha shambulizi hilo, ambapo mshambuliaji anadi kuwa mfuasi wa kundi la kigaidi la Islamic State.
Maelfu ya watu walikesha usiku kucha kuwakumbuka watu hao 49 waliuawa