WATUHUMIWA WA UBAKAJI WAFIKISHWA KORTIN NA KUSOMEWA MASHITAKA YAO

Watuhumiwa
wa Ubakaji Huko Dakawa,Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakipelekwa
Kortini Mjini humo kusomewa Mashtaka yao mapema leo.
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro imewapandisha kizimbani washtakiwa sita wakikabiliwa na mashtaka matatu tofauti, wakiwemo washtakiwa wawili wanaokabiliwa na mashtaka na kubaka na kumuingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yake binti mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Wami Dakawa Wilayani Mvomero.
Katika
kesi hiyo iliyovuta hisia ya mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro,
washtakiwa Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa Njombe na Zuberi Thabit (30)
mkazi wa Mbarali Mbeya wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya mkoa wa Morogoro Mary Moyo, wakikabiliwa na shtaka la kubaka
na kulawiti, wanalodaiwa kutenda aprili 27 mwaka huu majira ya usiku
katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo Wami Dakawa wilayani
Mvomero.
Upande
wa Serikali katika shtaka hilo lililofanyika faragha kwa mujibu wa
sheria, umewakilishwa na waendesha mashtaka Gloria Rwakibalila, Edgar
Bantulaki na Calistus Kapinga. Washtakiwa wote wawili wamekana mashtaka na kesi hiyo imepangwa kufikishwa tena Juni Mosi mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Upande wa mashtaka umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwa ajili ya usalama wa washtakiwa kwa vile shauri hilo limegusa hisia ya jamii na kwa vile upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa wanaweza kuharibu upelelezi.
Upande wa mashtaka umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwa ajili ya usalama wa washtakiwa kwa vile shauri hilo limegusa hisia ya jamii na kwa vile upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa wanaweza kuharibu upelelezi.
Katika
shtaka jingine lililofikishwa mbele ya Hakimu Ivan Msaki wa Mahakama
hiyo, washtakiwa sita wakiwemo Iddi Mabena, Zuberi Thabiti na wengine
wanne Rajab Salehe, Ramadhani Ally Makunja anayetetewa na wakili Ignas
Punge, Muhsin Ngai na John Petter maarufu kama Paroko, wakazi wa Wami
Dakawa wilayani Mvomero wanadaiwa kusambaza picha chafu na za ngono kwa
njia ya mtandao kinyume na sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya mwaka
2015.
Washtakiwa
wote sita wamekana mashtaka ambapo upande wa mashtaka ukiongozwa na
mawakili watatu wa serikali uliomba washtakiwa wanyimwe dhamana kwa
usalama wao na kutoharibu upelelezi kwa vile bado haujakamilika, huku
ule wa mshtakiwa namba nne ukiomba kuwasilisha kiapo cha kupinga
mshtakiwa kunyimwa dhamana, ambapo suala hilo la dhamana katika shauri
hilo litafikishwa tena juni mosi kwaajili ya kujadiliwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.
No comments:
Post a Comment