UWANJA WA NDEGE MWANZA UJENGWE KISASA ILI KUINUA SEKTA YA UTALII.
Na Tiganya Vincent-MAELEZO, Dodoma.
BAADHI
ya Wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa wameomba Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi
na Mawasiliano kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha
Kimataifa ili kuimarisha sekta ya Utalii na usafiri wa anga katika kanda
ya Ziwa.
Walisema
kuwa hatua itasaidia watalii wanaokuja nchini kushuka moja kwa moja
mkoani Mwanza na kisha kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na
maeneo mengine ya vivutio vya hapa nchini bila kupitia nchi jirani.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Wabunge Dkt.Raphael Chegeni na Mhe. Ezekeil
Maige wakati wakichangia hotuba kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara
ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha.
Mhe.
Dkt.Chegeni alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni muhimu ukajengwa
kwa viwango vya Kimataifa ili uweze kuruhusu ndege mbalimbali kubwa na
ndogo kuweza kutua bila tatizo.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia kuunganisha Mkoa wa Mwanza na nchi jirani za
Rwanda, Uganda na Burundi na hivyo kuruhusu ndege nyingi kutoka Nchi
hizo kutua bila kwenda katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mhe.
Dkt. Chegeni aliongeza kuwa uwanja huo endapo utajengwa kwa kiwango
cha Kimataifa utasaidia kuwa kiungo muhimu kwa mikoa 10 ya kanda ya
ziwanana kati.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Maige alisema kuwa ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Mwanza sio tu utasaidia kuunganisha mkoa huo na mikoa mingine
bali utasaidia kuchochea uchumi wa eneo la Kanda ya Ziwa na Tanzania
kwa ujumla kwani watalii na wasafiri wengine watakuwa na fursa ya
kuingia Mwanza bila kupitia nchi jirani.
No comments:
Post a Comment