Licha ya kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa GD Esperanca, Yanga imetinga hatua ya Makundi Kombe la CAF

Siku 11 baada ya klabu ya Dar es Salaam
Young Africans kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya mtoano ya 16 ya
Kombe la shirikisho barani Afrika CAF, Leo May 18 2016 Yanga waliifuata
GD Esperanca ya Angola kucheza mchezo wa marudiano, katika mchezo huo
Yanga imekubali kipigo cha goli 1-0.
Goli ambalo lilifungwa na Kabungula
dakika ya 25, kwa matokeo hayo Yanga wanafanikiwa kutinga hatua ya
Makundi ya Kombe la shirikisho barani baada ya kuitoa Esperanca kwa
jumla ya goli 2-1, hiyo inatokana na Yanga kuifunga Esperanca goli 2-0
katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment