KATIBU MKUU WA UCHUKUZI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA KATIKA MTAMBO WA KUPIMA MAFUTA (FLOW METER) BANDARI YA DAR ES SALAAM
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi, Mhandisi
Dk. Leonard Chamuriho amesema kuwa kasoro ambazo zimejitokeza katika
mtambo wa kupima mafuta Bandarini (Flow Meter) zinapatiwa ufumbuzi na
mkandasi wa vifaa vya mitambo hiyo.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Chamuriho amesema
kuwa mtambo huo lazima uangaliwe kwa umakini kutokana na serikali ndipo
inapata kodi yake halisi ya mafuta yanayoshuwa na meli.
Amesema
kuwa mkandarasi msambazaji vifaa kutokana na mkataba ni lazima
ahakikishe kwa vitu viliyopata kasoro kutatua kabla ya tatizo halijawa
kubwa au kutojirudia.
Aidha
amesema kuwa suala la kamera ambazo zimepata hitilafu baada ya kupigwa
na radi zitengenezwe mara moja na tatizo lisijirudie wakati mwingine
kutokana na umhimu wa kamera katika eneo hilo.
Amesema
kutokana hali hiyo amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari kupeleka taarifa
jumatatu ikiwa na ina vitu vyote ambavyo vipo katika mradi wa mtambo
huo.
Kwa
upande wa Meneja Mradi Mtambo wa kupima mafuta, Mhandisi Mary Mhayaya
amesema kuwa jana kumetokea changamoto katika mtambo iliyotokana na
mafuta kukwama kutokana na uchafu ambapo wameweza kusafisha.
Aidha amesema katika majaribio wa mtambo huo umeweza kuwa na mafanikio baada ya meli tatu kushusha mafuta bila matatizo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi, Mhandisi
Dk. Leonard Chamuriho akipata maelekezo kutoka kwa Meneja Mradi wa
Mtambo wa Kupima Mafuta wa TPA, Mhandisi Mary Mhayaya leo wakati ziara
kushtukiza na katibu Mkuu huyo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano –Uchukuzi, Mhandisi
Dk. Leonard Chamuriho akiwa juu ya mtambo akiangalia miundombinu yake
wakati wa ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kupima mafuta Kigamboni,
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment