Na Hamidu Abdallah
Dar es salaam
Halmashauri ya manispaa ya Ilala inatarajia kupitisha msako
wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani
wafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga watakaokiuka agizo
walilopewa na halmashauri hiyo.
Halmashauri hiyo imetoa agizo kwa kwa wafanyabiashara hao
kuondoka na kuacha kufanya biashara zao katika viunga vyote vya jiji na kwenda
katika maeneo waliyopangiwa ili kuacaha utamaduni wa kufanya biashara
barabarani kwa kuepusha misangamano na kuacha jiji safi.
Hayo yalibainika Mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi
wa halmashauri hiyo ambapo Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala Isaya Mngurumi alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari juu ya agizo hilo.
“Tumewapa siku tatu yaani kuanzia leo ijumaa waje kwa afisa
mipango miji wea halmashauri ili waelekezwe pakwenda na mwisho jumaapili ikifika jumaatatu tunaanza msako wa
kuwakamata watakao kaidi”, alisema Mkurugenzi Mngurumi.
Mkurugenzi Mngurumi alibainisha kuwa Jumla ya masoko mannne
yenye uwezo wa kuwaweka wafanyabiashara zaidi ya 6000 yametengwa ambayo ni soko la Kigogo
freshi lenye uwezo wa kuwa na wafanyabiashara 1500, soko la Tabata muslim uwezo
wake wafanyabiashara 1166, soko la Kivule lenye uwezo wa kuwa na wafanya
biashara 1000 na soko la Ukonga na lenye uwezo wa kuwa na wafanyabiashara 1500.
Na leo ndio jumaatatu ya zoezi kuanza ambapo msako huo
utahusisha wafanyabiashara wasio n maduka maalum, wanaopanga kando kando mwa
barabara za wapita kwa miguu na wale wanaopanga biashara zao katika barabara za
mabasi yaendayo kasi maarufu kama DAT.
Msako huo utafanywa na kamati ya ulinzi na usalama wa
halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na jeshi la polisi na mgambo
wa jiji wa JKT hivyo wafanyabiashara hao wametakiwa kutii agizo bila ya shurti.
No comments:
Post a Comment