Mwanamke mmoja katika muungano wa
milki za kiarabu amepigwa faini na kurudishwa kwao baada ya kupatikana
akiingia katika faragha ya mumewe.
Vyombo vya habari vinasema kuwa
mwanamke huyo alichukua na kufungua simu ya mumewe baada ya kumshuku
kwamba alikuwa na uhusiano wa kando.
Mumewe alilalamika kwa
maafisa wa polisi na mkewe akashtakiwa chini ya sheria ya uhalifu wa
mtandaoni, kulingana na chombo cha habari cha Gulf News.
Mwanamke huyo ambaye jina lake lilibanwa na ambaye ni mgeni katika muungano wa milki za kiarabu alipigwa faini ya pauni 28,000.
Alikiri
mahakamani kwamba aliifungua simu ya mumewe bila ya ruhusa na kuzituma
picha katika simu yake wakili wake aliiambia Gulf News.
Wakili
huyo Eman Sabt,alisema kwamba wanandoa hao walikuwa na umri wa miaka ya
30 na wenye asili ya kiarabu,lakini hakutoa maelezo zaidi
No comments:
Post a Comment