VYANZO VYA MAPATO VYA SERIKALI VIANGALIWE UPYA –CAG
Naibu
Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan
Mlay akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya CAG leo
jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan
Mlay akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa
ofisi ya CAG leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
OFISI
ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali imeitaka serikali kuangalia
upya vyanzo vyake vya mapato na matumizi ya fedha kwa sasa sio nzuri.
Akizungumza
katika mkutano wa kwanza wa Baraza jipya la wafanyakazi wa ofisi hiyo,
Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad
hiyo ni changamoto ambayo inapaswa kuangaliwa na kutafutiwa ufumbuzi na changamoto
zinazoikabili ofisi yake, amesema kuchelewa kupokea mgao wa fedha za
miradi ya maendeleo kwa wakati inasababisha ofisi hiyo kushindwa
kutekeleza mipango na kukamilisha miradi husika kwa wakati.
Profesa
Assaad amesema idadi ya watumishi iliyokuwepo katika ofisi yake
ilikuwa 81 ikaongezeka hadi kufika 150 lakini bado wanahitaji watumishi
wengine 129 wenye fani ya ukaguzi.
Aidha
amesema kuwa kulingana na weledi wa wakaguzi hao Tanzania imeteuliwa
kukaimu nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa
nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na China iliyomaliza muda wake mwaka
2014.
Nae
Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora ,
Susan mlay amesema watumishi wanatakiwa kuwa na weledi katika kufanya
kazi ili kuleta tija kwa taifa ikiwa pamoja na kuangalia masilahi yetu
kutokana na kazi wanazozifanya.
No comments:
Post a Comment