kufuatia mauwaji ya watu saba Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu atoa saa 24 kuwatia nguvuni wale wote waliohusika
Mhe.
Makamu wa Rais leo ametembelea Wilaya ya Sengerema kata ya Sima ambapo
usiku wa kuamkia jana kulifanyika mauwaji ya kinyama ya watu saba wa
familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu
wasiojulikana.Mhe. Makamu wa Rais Mama Suluhu Hassan ametoa masaa 24 kwa
uongozi wa mkoa wa Mwanza pamoja na jeshi la polisi na vyombo vingine
kuwatia nguvuni wale watu wote waliohusika na mauaji hayo.
Pichani ni makaburi yakiandaliwa kwa ajili ya kuzikwa kwa miili saba ya familia moja mapema leo Wilayani Sengerema .

Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu akisalimiana na kuwapa pole ndugu jamaa na
marafiki kufuatia mauaji hayo ya watu saba wilayani Sengerema

Mkuu
wa Wilaya ya Sengerema Bi Zainab Telack pamoja na Mkuu wa mkoa wa jiji
la Mwanza Mh.John Mongella wakiwa na Mgeni wao Makamu wa Rais Mh.Samia
Suluhu alipokewenda kutoa pole kwenye tukio la mauwaji ya kinyama ya
watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa
mapanga na watu wasiojulikana ndani ya wilaya hiyo katika kijiji cha
Sima mkoani Mwanza .
Makamu
wa Rais Mh Samia Sulluh akizungumza kwenye tukio la mauwaji ya kinyama
ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto zake kuuwawa kwa kukatwa
mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Mh.Samia ametoa saa 24 kukamatwa
kwa wale wote waliohusika na tukio hilo la Kinyama
No comments:
Post a Comment