Bao lililofungwa na Danielle carter
lilikisaidia kikosi cha wanawake wa timu ya Arsenal kuchukua taji la 14
la kombe la FA baada ya kutawala mechi dhidi ya Chelsea katika uwanja wa
Wembley.
Carter,ambaye alipiga juu alipopata nafasi yake ya kwanza aliipatia the Gunners uongozi baada ya kuvamia lango la Chelsea.
Asisat Oshoal baadaye alikosa fursa tatu za wazi kuongeza ushindi huo wa Arsenal.
Fran
Kirby alipoteza nafasi ya wazi ya kusawazisha kutoka upande wa Chelsea
katika mechi ya fainali iliohudhuriwa na mashabiki 32,912.
Mshambuliaji
huyo wa Uingereza alikosa mwelekeo katika kipindi cha kwanza na
hivyobasi kumpatia fursa kipa sari Van Veenendaal kuokoa mikwaju yake.
No comments:
Post a Comment